Image
Image

Wajumbe zaidi ya 200 wa kada ya sheria kutoka nchi mbalimbali za Afrika kukutana jijini Arusha.

Wajumbe  zaidi ya 200 wa kada ya sheria kutoka nchi mbalimbali za Afrika, wanatarajia kuhudhuria mkutano wa siku tatu wa majadiliano kuhusu masuala ya sheria Barani Afrika unaoanza kesho-kutwa Jijini  Arusha.
Majadiliano hayo ambayo, yanaratibiwa kwa ushrikiano baina ya Mahakama ya Afrika ya Haki za binadamu na a watu,  yenye makao yake makuu Jijini Arusha na Umoja wa Afrika, yatawajumuisha  majaji wakuu wa nchi husika, Marais wa Mahakama za juu na Mahakama za Katiba,wasomi na watendaji wengine wa Mahakama za Kitaifa.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Rais wa Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu na watu, Jaji Mkuu Mstaafu wa Tanzania,  AUGUSTINO RAMADHAN imesema  majadiliano hayo ya masuala ya sheria Barani Afrika hufanyika mara moja kila baada ya miaka miwili.
Ameitaja  kauli mbiu ya majadiliano hayo kuwa ni  'Kuunganisha Sheria Za Kitaifa Na Zile Za Kimataifa' ,ni ufuatiliaji wa majadiliano ya kwanza ya aina hiyo yaliyofanyika Jijini  Arusha mwaka 2013.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment