Raia mmoja wa Rwanda ambae alihamia
nchini Ujerumani mwaka 2002 amehukumiwa kifungo cha maisha gerezani baada ya
kukutwa na hatia ya kushiriki kataika mauaji ya kimbari yaliotokea nchini
Rwanda mwaka 1994.
Muhukumiwa Onesphore Rwabukombe
amekana kuhusika na shutuma hizo za mauaji yaliosababisha vifo vya watu 400
mashariki mwa Rwanda.
Kabla ya hukumu hiyo kutolewa,
alihukumiwa kifungo cha miaka 14 kwa mauaji ya watu 450 ambao walikimbilia
kujificha katika kanisa la Kiziguro mashariki mwa Rwanda.
Mahakama hiyo ilifahamisha baada ya
kukusanya ushahidi kuwa Onesphore Rwabukombe aliwasafirisha wanamgambo wake
katika gari lake hadi katika eneo la tukio na kutekeleza mauaji.
0 comments:
Post a Comment