Kampuni ya masoko ya michezo inaaminika kulipa mamilioni ya dola za Kimarekani kwa maafisa waandamizi wa FIFA katika miaka ya mwishoni mwa 1990 ili kupewa haki ya kutangaza michuano ya kombe la dunia.
Aliyekuwa ameshikia nafasi hiyo kabla ya Blatter, Joao Havelange, alikuwa ni miongoni mwa wanaotuhumiwa kupokea malipo hayo.
Bwana Blatter, amekana kuwa na taarifa yoyote ya sakata hilo, lakini kipindi cha Panorama kimeona barua iliyosainiwa na bwana Joao Havelange ikisema bwana Blatter ana taarifa kamili.
0 comments:
Post a Comment