Kichapo hicho, ambacho ni cha nane katika mechi 15 Ligi ya Premia, kimewaacha mabingwa hao watetezi wakiwa alama 14 nyuma ya Manchester United walio nambari nne.
"Lengo letu ni kumaliza katika nne bora," alisema Mourinho.
"Kabla ya mechi hii, kulikuwa na msingi kufikiria kuwa tulikuwa na uwezo wa kujitoa katika hali hii lakini sasa, labda, itatubidi kufikiria kuhusu sita bora.”.
Chelsea kwa sasa wamo alama tatu juu ya eneo la kushushwa daraja, na alama 17 nyuma ya viongozi wa ligi Leicester.
Mourinho aliongeza: "Nina wasiwasi bila shaka. Lakini hakuna uwezekano kwamba mwishoni mwa msimu Chelsea itakuwa ikipigana kuzuia kushushwa daraja.
0 comments:
Post a Comment