Image
Image

Burkina fasso yatoa hati ya kukamatwa kwa Rais wa zamani wa nchi hiyo Blaise Compaoré.




Serikali ya Burkina fasso imetoa  hati ya kukamatwa kwa Rais wa zamani wa nchi hiyo Blaise Compaoré  kwa tuhuma za mauaji ya Rais mwingine wa zamani wa nchi hiyo Thomas Sankara  tukio alilolifanya miaka 30 iliyopita.
Mwanasheria wa familia ya Marehemu Sankara aitwaye Prosper Farama  amesema katika hati  hiyo Bw.Campaore  anatuhumiwa kuhusika na mauaji hayo yaliyoenda sambamba na kuipindua Serikali iliyokuwa chini ya Marehemu Sankara.
Sankara aliuawa mwaka 1987 sambamba na wafuasi wake 12 kitendo kilichosababisha umwagaji wa damu nchini humo Burkina Faso yaliyodumu kwa siku kadhaa kabla ya kumalizika kwa Bw.Blaise Compaoré  kuingia madarakani kuiongoza nchi hiyo katika wadhifa wa Urais.
Blaise Campaore ambaye kwa sasa anaishi uhamishoni nchini Ivory Coast aliachia madaraka ya  Urais wa Burkina faso octoba mwaka jana baada ya jaribio lake la kutaka kubadilisha katiba ya nchi hiyo na kujiongezea muda wa kukaa madarakani kushindikana.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment