Kauli hiyo ya CUF imetolewa na
kaimu mkurugenzi wa habari na Mawasiliano na Umma Bw.Ismail Jussa wakati
akiongea na waandishi wa habri ikiwa ni siku moja tu baada ya CCM kupitia kikao
chake cha halmashuri kuu ya Zanzibar ya CCM kutoa tamko la kuwataka wana CCM
kujiandaa na marudio ya uchaguzi ambapo kiongozi huyo wa CUF amesema kauli ya
CCM ni ya chama kilichoshindwa na kuwahadaa wananchi huku ikiwahakikishia
wanachama na wananchi kuwa CUF italinda matokeo halali ya uchaguzi.
Akizumgumzia mazungumzo yanayoendelea
hivi sasa kuhusu mvutano wa mgogoro huo wa kisiasa Zanzibar kaimu mkurugenzi
huyo wa habari Ismail Jussa amesema hatua iliyofikiwa ni kubwa na yako
katika hatua za mwisho huku CUF ikiwapongeza wananchi kwa kuonyesha
ukomavu wa kisiasa na kundeleza hali ya amani na utulivu.
CCM na CUF ambavyo ndivyo vyama vikuu
vya kisiasa hapa Zanzibar zinaonekana kuzidi kuwachnaganya wananchi ambao
sasa wameingia mwezi wa pili tokea kufutwa kwa matokeo ya uchaguzi na
zaidi ya mara sita kwa kamati inayosimamia mggooro huo ambao ina wagombea
wawili wa urais wa CCM na CUF na marais wastaafu wa Zanzibar kukutana na hadi
sasa hakuna kauli yeyote iliyotolewa.
0 comments:
Post a Comment