Siku moja baada ya viongozi wa dunia kuonyesha dhamira ya kuungana
katika kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabia nchi, wajumbe wa
mkutano wa Umoja wa Mataifa wanaendelea na mazungumzo muhimu.
Wakuu wa mataifa zaidi ya 150 wamekusanyika katika viunga vya jiji la
Paris tangu Jumatatu katika jitihada ya kuchapua kasi ya kisiasa katika
kile ambacho wengi wamekielezea kuwa fursa ya mwisho ya kuepusha madhira
ya mabadiliko ya tabia nchi.
Wakati wa ufunguzi kiongozi mwenyeji wa mkutano huo Francois Hollande
amenukuliwa akisema "Matumaini yote ya ubinaadamu yapo katika jitihada
zetu".
Marais Barack Obama na mwenziwe wa China Xi Jinping sambamba na
viongozi wengine wengi waliapa, kwamba mataifa yao yatapambana kudhibiti
hewa chafu, ambayo inasababisha ongezelo la joto duniani. Wameahidi
kwamba matokeo ya mkutano huo wa mabadiliko ya tabia nchi yatakuwa
kuwepo kwa mkataba wa 2020, ambao utausaidia ulimwengu na vizazi
vijavyo.
Rais Obama ambaye leo hii(10-12-2015) anatarajiwa kukutana na viongozi
wa visiwa ambavyo vipo hatarini kuzama kutokana na kuongezeka kwa kina
cha bahari alisema "Hatma ni moja, ambayo tuna nguvu ya kuibadili, hapa
hapa na sasa hivi". Katika mkutano huo Obama atawaelezea viongozi hao
jukumu lake katika kusaidia vile visiwa vilivyo katika mazingira magumu
sana.
Lakini ahadi kama hizo zilitolewa katika mkutano kama huo wa mazingira wa Umoja wa Mataifa zaidi ya miongo miwili iliyopita.
wasiwasi wa mafanikio
Mchakato wa Umoja wa Mataifa unaoshughulikia mabadiliko ya tabia nchi
unakabiliwa na wasiwasi kuhusu matumizi ya nishati ya mafuta, kama
tegemeo la dunia na kwamba kutokana na jambo hilo maslahi makubwa
yatakuwa hatarini. Kwa miaka kadhaa katika mikutano mikubwa ya
mabadiliko ya tabia nchi kumekuwa vitendo vya kunyoosheana vidole, hasa
kati ya mataifa tajiri ya masikini juu ya nani hasa anapaswa kubeba
mzigo wa uchafuzi wa mazingira.
Mvutano huo umeibuka wazi kabisa hata Jumatatu, siku ya kwanza ya
mkutano wa kilele wa maadiliko ya tabia nchi pale ambapo mataifa
yanayoendelea yalipoyashambulia mataifa yalioendelea yapohimiza
kupunguzwa kwa matumizi ya nishati ya mafuta baada ya wao kupata
mafaniko kwa kutumia nishati hiyo hiyo iliyosababisha kiwango kikubwa
cha uchafuzi wa mazingira duniani.
Katika hatua nyingine rais wa Ufaransa, Francois Hollande anafanya
mkutano na viongozi wa Afrika wenye lengo la kutaka kujua mataifa hayo
yanahitaji nini hasa katika kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchini na
kupunguza ongezeko la joto duniani.
Mkutano huo wa leo, ni sehemu ya jitihada pana ya kidemokrasia yenye
lengo la kufanikisha makubaliano ya muda mrefu yanayowezekana kufanyika
kwa mtaifa yote ya Afrika, kudhibiti uzalishaji wa hewa chafu unaofanwa
na mwanadamu. Wanasayansi wanasema hewa hizo zinasababisha mgamdo wa
gesi ambayo inasababisha kuyeyuka kwa barafu na kiwango cha bahari
kuongezeka na kuongeza hali ya ukame na majanga mengine.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment