Image
Image

Viungo Kili Stars wanakibarua kigumu kuichinja Ethiopia leo.

Kilimanjaro Stars itakuwa na kibarua kigumu itakapowakabili wenyeji Ethiopia katika mechi ya robo-fainali ya michuano ya Kombe la Chalenji itakayochezwa kwenye Uwanja wa Taifa wa Addis Ababa jijini hapa leo. 
Timu hiyo inayonolewa na kocha mzalendo, Abdallah ‘King’ Kibadeni, itakutana na wenyeji kwa mara ya pili baada ya juzi timu hizo kutoka sare ya 1-1 katika mchezo wa mwisho wa Kundi A.

Kikosi cha Stars cha leo hakitakuwa na mabadiliko makubwa, lakini Kibadeni aliweka wazi jana kuwa ataongeza kiungo mkabaji ili kuwadhibiti wapinzani wao ambao wanacheza mpira wa kushambulia mfululizo.

Alisema amepanga kusaka matokeo ya mapema katika mchezo wa leo ambayo yataweza kuisaidia timu yake kupunguza presha itakayoweza kujitokeza endapo wataingia kipindi cha pili bila ya kupata bao la kuongoza.

Katika mazoezi yake ya jana, Kabdeni alionekana kuwafundisha na kuwajengea nyota wake uwezo wa kupiga pasi makini na za uhakika.

Mshauri wa kiufundi wa timu hiyo, Boniface Mkwasa ambaye pia yupo jijini hapa, alisema: “Kilimanjaro Stars wana kila sababu ya kushinda mchezo wa kesho (leo) dhidi ya Ethiopia maana wana kikosi kikubwa na chenye wachezaji wenye uwezo wa kusaka ushindi.

“Kiufundi tumewazidi sana Ethiopia, uwezo wa wachezaji wao na wale wa kwetu ni tofauti, tuna kikosi kizuri na tumejipanga kupambana kesho bila kuwabeza.”

“ Nina kazi kubwa ya kuiangusha Tanzania. Ninaiheshimu na ninafahamu kuwa ni moja ya timu bora kwenye mashindano haya, nitapambana na kuhakikisha tunapata ushindi,” Kocha wa Ethiopia, Sahili Yohannes alisema jana.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment