Image
Image

Andrey Coutinho kuuzwa kwenye klabu ya St. George ya Ethiopia.

Andrey Coutinho alianza mazoezi jana kwenye kikosi cha Yanga, lakini mabingwa hao mara 25 wa Bara wamepanga kumuuza kiungo huyo wa kimataifa kwenye klabu ya St. George ya Ethiopia, imefaamika.
Coutinho alireja nchini juzi akitokea kwao Brazil alikokwenda kwa ajili ya mapumziko baada ya ligi ya Bara kusimama kwa muda kupisha mechi za Taifa Stars dhidi ya Algeria na michuano ya Chalenji.
Mmoja wa viongozi wa benchi la ufundi la Yanga, aliiambia Nipashe jana kuwa kwa sasa Yanga wanasubiri St. George ikamilishe tu taratibu za usajili ili wamruhusu mchezaji huyo.
"Coutinho anaondoka, kwa sasa wanasubiriwa St. George waje, na muda wowote wakikamilisha mambo, tutaachana naye," alisema kiongozi huyo ambaye aliomba hifadhi ya jina lake kwa kuwa si msemaji wa klabu hiyo ya Jangwani.
Alisema tayari mchezaji huyo amepewa taarifa ya mpango huo wa kuuzwa na kwamba kuondoka kwake, kutatoa nafasi kwa kocha mkuu Hans van der Pluijm kuongeza mchezaji mwingine wa kimataifa Jangwani.
Kikosi cha Yanga kinaendelea na mazoezi kwenye Uwanja wa Boko Veteran jijini Dar es Salaam kujianda kwa mwendelezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara. Timu hiyo inayotetea ubingwa, itacheza michezo miwili mfululizo mkoani Tanga dhidi ya African Sport na Mgambo Shooting Desemba 12 na 16.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment