Hospitali ya rufaa ya KCMC mkoani Kilimanjaro inakabiliwa
na tatizo la vitanda vya kufanyia upasuaji hali ambayo inazidi kuchangia
ongezeko la msongamano wa wagonjwa wodini huku baadhi ya wagonjwa wakilazimika
kulala kwenye varanda kusubiri huduma.
Mkurugenzi wa hospitali ya rufaa ya KCMC Prof Giliad
Masenga ameyasema hayo wakati akipokea msaada wa Blanketi maalumu za wagonjwa
kutoka benki ya Diomond Trust na kuwa vitanda vinavyotumika kwa sasa ni
chakavu.
Amesema idadi ya wagonjwa wanaofanyiwa upasuaji ni kubwa
na kwamba vitanda vilivyopo ni vya zamani na kwamba ununuzi wa vitanda hivyo ni
gharama kubwa ambapo kitanda kimoja kinagharaimu zaidi ya shilingi milioni 40.
Mapema akikabidhi shuka hizo maalumu za wagonjwa 100
zenye thamani ya shilingi milioni 5 kati ya shuka 2000 zinazohitajika
hosptalini hapo meneja wa benk ya Diomond Trust tawi la Moshi Bw.John Robert
amesema msaada huo ni sehemu ya faida waliyopata na kutokana na kazi
wanayoifanya.
Akizungumzia hali ya msongamano wa wagonjwa katika
hospitali hiyo afisa uhusiano wa hospitali ya rufaa ya KCMC Bw.Gabriel Chiseo
amesema tayari wako katika hatua za mwisho za kukamilisha ujenzi wa idara ya
wagonjwa wa dharura ambayo inatarajia kuanza kutumika mwezi January mwakani
2016.
0 comments:
Post a Comment