Image
Image

Latest News:Gari ya Magazeti ya Mwananchi imepata ajali na kusadikiwa kuua.

Kupitia mitandao ya kijamii hususani kwenye facebook, whatsapp na Instagram imeenea taarifa inaonekana gari ya magazeti ya mwananchi imepata ajali na kunatajwa kuwa kuna watu wamefariki pia kwenye ajali hiyo.
Nimempata Mhariri wa gazeti la Mwananchi, Frank Sanga ambaye amesema yuko mkoani Tanga kikazi lakini taarifa alizozipata ni kwamba gari lililopata ajali ni gari ambalo lilikodiwa na Kampuni hiyo ya Magazeti kupeleka Magazeti Mbeya… mazingira ya ajali inaonesha gari hilo liligonga lori kwa nyuma, na madereva wote wawili waliokuwa ndani ya gari wamefariki.
Ajali hiyo imetokea maeneo ya mlima Kitonga mkoa wa Iringa.
Chanzo: Millard ayo.com
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment