Image
Image

Breaking News:Watuhumiwa wanane wa upotevu makontena 349 wapandishwa Kisutu


Watuhumiwa wanane wa upotevu wa makontena 349 Bandarini wamefikishwa katika mahakama ya Hakimu mkazi Kisutu wakikabiliwa na makosa mawili ikiwemo,Kulanjama na kudanganya pamoja na kuisababishia hasara serikali ya shilingi bilioni 12.7.
Kukabiliwa kwa makosa hayo ni kufuatia kudanganya serikali juu ya makontena hayo 349 kuwa yametolewa katika bandari ya nchi kavu ambayo ipo eneo la Azam Dar es Salaam na kusema kwamba tayari limekwisha lipiwa kodi ya serikali.
Shitaka la pili wanalokabiliwa nalo la kuisababishia hasara serikali nikutokana na kushindwa kufanya majukumu yao kama inavyotakiwa hivyo kuweza kufikishwa katika mahakama ya kisutu.
Kwa mujibu wa hakimu anayesikiliza kesi hiyo amesema kuwa mahakama hiyo haina mamlaka ya kusikiliza wala kutoa dhamana wenye mamlaka pekee ni mahakama kuu kwa maana hiyo washitakiwa hao baada ya kusomewa mashtaka yao sasa wamerudishwa rumande mpaka tarehe 17 Disemba mwaka 2015,ambapo itatajwa tena.
Katika mahakama hii ya kisutu ndugu jamaa na rafiki walifika hapo kwa lengo la kujua ndugu zao watapata dhamana hali iliyokuwa tofauti baada ya mahakama hiyo kutokuwa na uwezo wa kutoa dhama kwa kesi hiyo hadi mahakama kuu pekee.
Endelea kufuatilia Taarifa zetu kufahamu zaidi,Like Page yetu uwe wakwanza kupata habari.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment