Image
Image

Waliokuwa wafanyakazi wa Mahakama ya kimbari ya Rwanda wadaui haki zao.

Siku chache baada ya Mahakama  ya  Kimataifa ya kushughulikia mauaji ya kimbari  ya  Rwanda  kutangaza  kufunga  shughuli  zake hapa nchini baadhi ya waliokuwa wafanyakazi katika mahakama hiyo wamefungua kesi  katika taasisi ya kushughulikia haki za wafanyakazi  wakidai  kulipwa zaidi ya Dola Laki-Nane za Marekani  kama stahiki zao za  kuachishwa kazi .
Wawakilishi wa wafanyakazi  hao  wa mesema kwa muda mrefu  wamekuwa  wakifuatilia  haki  zao  bila  mafa nikio  na  wameona kuwa njia pekee  ni  kufungua kesi  na  ameviomba  vyombo vingine  vinavyosimamia  haki kuwasaidia .
Akizngumzia  malalamiko  hayo ,  wakili   anayewasaidia,kutoka Kituo  cha Sheria na Haki  za Binadamu,tawi  la Arusha,SHILINDE  NGALULA amesema malalamiko  ya  wa fanyakazi hao yana  msingi  na wanastahili  kulipwa haki  zao kwani ndivyo  sheria  inavyoelekeza .
SHILINDE amesema inasikitisha  kuona chombo  kikubwa  na  kinachotegemewa kimataifa kusimamia haki  kinalalamikiwa  kuwa  sehemu  ya  kuanza  kukiuka  haki hizo .
Mahakama  hiyo iliyokuwa na makao yake makuu Jijini Arusha kwa zaidi ya miaka 20  sasa  imemaliza majukumu yake ya kushughulikia  watu humiwa  wa  mauaji ya  kimbari ya  Rwanda .
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment