Image
Image

Latest News:Kiwanda cha urafiki chafungwa kwa kushindwa kulipa wafanyakazi stahiki zao.

Uongozi wa wilaya ya kinondoni umesitisha shughuli za uzalishaji katika kiwanda cha urafiki baada ya viongozi wa kiwanda hicho kushindwa kuwalipa madai yao kama walivyokubaliana awali kuwa hadi Desemba 1 wangekuwa wameshalipwa.

Wafanyakazi hao ambao awali waligoma ili kushinikiza uongozi wa kiwanda hicho kuwalipa stahiki zao wamegoma tena hali iliyosababisha uongozi wa wilaya kuchukuwa hatua hiyo hadi wiki ijayo serikali itakapokuwa imelipatia ufumbuzi suala hilo.

Katika kiwanda hicho wafanyakazi hao wameonekana wakiwa wamefunga geti na kuweka kambi nje ya eneo hilo kwa madai kuwa uongozi wa kiwanda uwaeleze hatima ya malipo yao.

Hata hivyo katika hali ya kushangaza viongozi wote wa kiwanda hicho hawakuwepo maofisini na milango ilikuwa imefungwa hata baada ya viongozi wa serikali kufika.

Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment