Waziri mkuu Mhe.Kassimu Majaliwa kwa mara nyingine
amefanya ziara ya kustukiza kwa mifumo ya uingizaji na utoaji mizigo bandarini
na kubaini kotena za mizigo 2431 zinazomilikiwa na watu kumi tu zikiwa
zimeingizwa na kutolewa bandarini bila ushuru na kulikopesha taifa mapato ya
mabilioni ya shilingi.
Waziri mkuu Mhe.Kassimu Majaliwa aliyeingia kwa
staili ya kuanzia vitengo vidogo vya kimfumo ya IT akihoji uwezekano wa mifumo
hiyo kuzuia wizi na utoroshaji wa makontena huku akilishwa maneno matamu na
viongozi wa bandari akiwemo meneja wa bandari Bw.Abel Muhanga kuwa kwa mifumo
hiyo kuwa hakuna uwezekano wa mtu yoye kupitisha mzigo bila kulipa ushuru.
Hali hiyo ilibadilika mara baada ya waziri mkuu
Kassimu Majaliwa kutoa ripoti ya ukaguzi wa Marchi hadi Desemba Mwaka jana kuwa
kontena 2532 zimethibitishwa na wakaguzi kuwa zimepitishwa bila kulipa ushuru
na konyeshwa majina ya wahusika hali ilioyoonekana kuwa shubiri kwa meneja wa
bandari akikiri kuwatambua na kujitetea kuwa angeambiwa baadae.
Katika hali hiyo Mhe.Majaliwa amemuagiza meneja wa
bandari kuwa hadi jioni ya leo awe amewasilisha majina yote ya wakweepaji kodi
wakubwa na hatua za kisheria zichukuiwe mara moja.
Aidha Mhe.Majaliwa alipita shiirika la reli TRL
kukagua miradi ambapo amesikika akitoa kauli ya kuwashutumu kutumia zaidi ya
shilingi bilioni 200 isivyo tarajiwa.
0 comments:
Post a Comment