Maafisa wa Mamlaka ya Mapato nchini waliofanya ukaguzi wa awali katika makontena tisa yaliyokamatwa katika eneo la Mbezi Tanki Bovu Jijini Dar es Salaam wamebaini kuwa makonteina hayo yamelipiwa kodi na yametoka bandartini kwa kufuata utaratibu.
Makontena hayo yaliingizwa nchini kutoka China yakiwa na vifaa vya ujenzi.
Wahusika wa kusafirisha makontena hayo kampuni ya PMM ICD wamesema walilazimika kupeleka makontena hayo katika eneo hilo ili kuyahifadhi kabla ya kumfikishia mteja wao .
Mmiliki wa makontena hayo kampuni ya Heritage Empire Co Ltd , mbali na kueleza kuwa mali hiyo haina mashaka kwani imeingizwa nchini na kuondolewa bandari ni kwa kufuata taratibu zote , lakini alishikwa butwaa baada ya kuona makontena yake yamefikishwa katika eneo la Mbezi badala ya Bagamoyo ambako mradi wa ujenzi ulipo.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment