Katika kuiadhimisha siku hii mwandishi wetu Matthias von Hein anasema haki za binadamu zinahitaji hali ya hewa imar.
Katika mwaka huu pia pana sababu ya nguvu ya kusisitiza ulazima wa
kukomesha utekelezaji wa kupita kiasi wa adhabu ya kifo, nchini China,
Iran au Saudi Arabia.Pia ni wasaa wa kusisitiza juu ya kukomesha mateso,
ukatili unaofanywa na polisi na ukandamizaji wa uhuru wa kutoa maoni.
Lakini katika upande mwingine tunaweza kushangilia kutolewa mwaka
huu,kwa haki kabisa ,tuzo ya amani ya Nobel kwa jopo la mdahalo wa
kitaifa nchini Tunisia.
Katika kuiadhimisha siku ya haki za binadamu leo, pia inahalisi kabisa
kutoa mwito kwa viongozi wa wajumbe wanaoshikri kwenye mkutano wa
mazingira mjini Paris waache tofauti zao kando na waienzi ibara ya tatu
ya tamko la haki za binadamu ili iwe ya zama za leo. Ibara hiyo inalinda
haki ya maisha.
Athari za mabadiliko ya tabia nchi zinaua:
Watu wanakufa kutokana na madhara yanayotokana na mabadiliko ya hali
ya hewa. Wakati mwingine moja kwa moja. Kwa mfano hali mbaya kabisa za
hewa zimeongezeka kwa kiwango kikubwa.
Katika kipindi cha miaka 20 iliyopita wati nusu Milioni wamekufa
kutokana na mafuriko na dhoruba. Mambo ya hali ya hewa ni ya utata kiasi
kwamba haiwezekani kuzibainisha sababu zake kwa uhakika. Lakini hali
mbaya za hewa pia zinaua kwa njia nyingne. Kwa mfano kwa kuziyumbisha
nchi.
Mfano ni Syria. Vita vya nchini Syria, vilivyosababisha vifo vya maalfu
ya watu na kuwafanya mamilioni wengine wayahame makaazi yao,
vilitanguliwa na ukame.Wakulima Milioni moja na nusu walilazimika
kuyatelekeza mashamba yao na kukimbilia mijini, wakati ambapo Syria
ilikuwa tayari inalibeba zigo kubwa la mawimbi ya wakimbizi kutoka Irak.
Hata jamii imara ingelitetereka katika mazingira kama hayo.
Mabadiliko ya tabia nchi husababisha mashaka ya usalama: Nchini Syria
tatizo liliongezeka kutokana na utawala mbaya na uchochezi kutoka nje
Mfano mwingine ni Boko Haram. Siyo jambo la nasibu kwamba ujio wa Boko
Haram unahusiana na kukauka kwa ziwa Chad Ikiwa msingi wa maisha kwa
watu Milioni 30,wakulima, mafalahi,wafugaji na wavuvi unanywea na
kubakia asilimia 20 tu,mapambano ya kupigania raslimali yanakuwa
makali.Na ikiwa umaskini na hali ya kukata tamaa inaenea basi inakuwa
rahisi kwa makundi ya magaidi kuwaghilibu vijana.
Kupanda kwa joto kunasababisha mawimbi ya wakimbizi na ya wahamiaji kwa
viwango vikubwa. Na upatikanaji wa raslimali, na hasa maji huwa ngondo
mara nyingine.
Njaa itaongezeka duniani. Hata tajiri hawataweza kuwalisha watu wote.
Katika kila sekunde tatu anakufa njaa mtu mmoja duniani na aghalabu
mtoto. Asilani hatuwezi kuikubali hiyo. Jee ni kwa sababu ya mazoea tu
au kutokana na kukosekana kwa ubunifu wa kuujenga uchumi wa haki?
Nchi tajiri za viwanda lazima zitangulie mbele kwenye mkutano wa mjini
Paris.Wengine wafuate.Unaohusika hapa ni mustakabal wa mwanadamu.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment