Muda si mrefu Rais wa Tanzania awamu ya Tano
Dkt.John Pombe Magufuli amewaita wanahabari Ofisini kwake kwa lengo la
kuzungumza nao lakini haijafahamika mara moja nini anataka kuzungumza
nao.
Licha yakuwa haijabainika ninini anachotaka kusema
lakini kwa fununu na hamu iliyokuwa kubwa kwa watanzania wanabashiri kuwa
huenda akaliweka wazi baraza la mawaziri ambalo amekuwa akisema anataka liwe
dogo na lenye watendaji kazi wazuri ndani ya serikali yake ya awamu ya Tano
yenye kaulimbiu ya Hapa kazi tu.
Tangu kuchaguliwa kuwa Rais wa Tanzania ameweza
kufanya mambo mazito ndani ya nchi haswa kwa kugusa sehemu nyeti ndani ya
serikali hali ambayo imekuwa ikimfanya apate sifa ndani na nje ya nchi huku wengine
katika nchi zao wakitamani akawe rais katika nchi zao kwa kile wanachotaja kuwa
sasa Tanzania imepata mkombozi.
Licha ya kuwa hajatangaza baraza la mawaziri Rais
Magufuli lakini nchi imekwenda vizuri kwa kuwa na Waziri Mkuu,Kassim
Majaliwa,Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan,Mwanasheria mkuu wa Serikali George
Masaju,Spika wa Bunge Mh.Job Ndugai na Naibu Spika Tulia Ackson Mwansasu.
Kasi ya Rais Magufuli na Waziri wake imekuwa kubwa
kwa kutumbua Majipu katika Mamlaka za Kodi TRA na Mamlaka ya Bandari TPA, na
kulazimika kufuta Sherehe za Uhuru,Siku ya Maadhimisho ya Ukimwi,Kufuta Safari
za Nje nk.Kusudi kubana matumizi ya sio kuwa na Tija.
Itakavyokuwa baada ya Mazungumzo tutakufahamisha
kilicho jiri.
0 comments:
Post a Comment