MGOMBEA ubunge wa Jimbo la Arusha Mjini kupitia Chama Cha Demokrasia
na Maendeleo (Chadema), Godbless Lema, anaelekea kurejea tena bungeni
huku akimwacha kwa mbali mpinzani wake, Philemon Mollel wa Chama Cha
Mapinduzi (CCM).
Katika matokeo ya awali ambayo yalibandikwa vituoni katika baadhi ya
kata za Arusha, yanaonesha Lema anaongoza takribani katika vituo vyote,
jambo ambalo ni dalili za kuibuka kuwa mshindi wa nafasi hiyo ambayo
anaitetea kwa kipindi cha pili.
Pamoja na idadi ndogo ya wapiga kura waliojitokeza katika uchaguzi
huo tofauti na uchaguzi uliopita, haikumzuia Lema kuongoza katika
matokeo hayo ya awali ambayo yalibandikwa vituoni.
Matokeo hayo ya awali yanadhihirisha mwitikio wa wapiga kura wa
Arusha dhidi ya kauli iliyotolewa juzi na Waziri Mkuu wa zamani, Edward
Lowassa aliyewataka wananchi wa jimbo hilo kupiga kura kwa wingi.
Katika matokeo hayo ya awali Kata ya Daraja Mbili Chadema ilikuwa
imekwisha jihakikishia ushindi katika kata hiyo kwa kuibuka na kura
1,572 huku CCM ikiambulia kura 916.
Katika vituo vingine matokeo yalikuwa kama ifuatavyo. Kata ya Elerai
Kituo cha Shule ya Msingi Mama Mussa, kituo namba 1, CCM 69, Chadema 70,
Mama Musa namba 2, CCM 63 na Chadema 67, kituo cha Remtula namba 1
Chadema 56 na CCM 50, Remtula 2 Chadema kura 54 na CCM kura 35, kituo
cha Remtula namba 3 Chadema kura 68, CCM 66 na ACT kura 1 namba 4.
Chadema kura 46 na CCM kura 43
Kituo cha shule ya Msingi Elerai Majengo kituo namba 2 Chadema 67,
CCM 62, CUF 1, Majengo A Chadema kura 94, CCM kura 29, Majengo A1
Chadema kura 106 na CCM kura 34.
Mtaa wa Olkereyan Kata ya Olasiti kituo namba 2, waliopiga kura
walikuwa ni 151 ambapo Chadema ilipata kura 109, CCM kura 40, ACT kura 1
huku kura moja ikiharibika.
Katika Kata ya Levolosi, Shule ya Msingi Levolosi kituo namba 2
Chadema kura 100, CCM kura 48, ACT kura 0, CUF kura 0 na NRA kura 0.
Kata ya Olasiti Kituo cha Shule ya Msingi Olasiti kulikuwa na vituo
saba ambapo kituo cha kwanza Chadema kura 107, CCM kura 75 na ACT kura
1.
Kituo cha Pili Chadema kura 112, CCM kura 77, kituo namba tatu
Chadema kura 111, CCM kura 58. Kituo namba 4 ChademaA kura 102, CCM kura
87, kituo namba 5 Chadema kura 78, CCM kura 102, ACT kura 1, kituo
namba 6 Chadema kura 113, CCM kura 91, ACT 2, na kituo namba 7 Chadema
kura 81, CCM 73 na ACT kura 2.
Kituo cha Osunyai kulikuwa na vituo vitano ambapo kituo cha 1 Chadema
kura 123, CCM kura 59, kituo cha 2, Chadema kura 110, CCM kura 64,
kituo cha 3, Chadema kura 129, CCM kura 41, kituo cha 5, Chadema kura
103 CCM kura 50 na kituo cha 6 Chadema .kura 103 na CCM kura 49. Kituo
cha 7, Chadema kura 109 na CCM kura 44.
Katika Kituo cha Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Arusha Kata ya Sekei
mgombea wa Chadema aliibuka katika vituo vyote vitatu ambapo kituo cha
kwanza Chadema ilipata kura 115 na CCM kura 50, kituo cha pili Chadema
kura 67 na CCM 61, kituo cha tatu Chadema 76 na CCM kura 57.
Wasimamizi na WhatsApp
Katika hali ambayo haikutarajiwa baadhi ya wasimamizi na mawakala wa
vyama vya siasa katika Jimbo la Arusha Mjini walijikuta wakitumia muda
mwingi kuchati na simu ikiwamo kutumia mtandao wa kijamii wa ‘WhatsApp’
kutokana na idadi ndogo ya wapiga kura waliojitokeza katika vituo 721.
Pamoja na hali hiyo wengine walijikuta wakiwa wamepumzika kwenye
viti, huku wakiendelea kubadilishana mawazo wakati wakisubiri wapiga
kura.
Moja ya sababu iliyosababisha kujitokeza kwa idadi ndogo ya wapiga
kura vituoni, ni kuwapo kwa dalili ya mvua kubwa ambayo iliambatana na
wingu zito kutanda kuanzia saa 4 asubuhi na ilipofika saa 9 alasiri mvua
ilianza kunyesha.
Kutokana na hali hiyo watu wengi walijifungia ndani ya nyumba zao na
wengine walikuwa katika nyumba za Ibada au kumbi za starehe na kuupa
kisogo uchaguzi huo.
Handeni Mjini
Taarifa kutoka wilayani Handeni, zilizopatikana jana jioni wakati
tukienda mtamboni, zilieleza kuwa mgombea wa Chama Cha Mapinduzi (CCM),
Omari Kigoda, alikuwa akiongoza katika matokeo ya awali dhidi ya mgombea
wa Chama cha Wananchi (CUF), Remmy Shundi.
Katika matokeo hayo ya awali yanaonesha katika Kata ya Chanika, CCM
ilikuwa ikiongoza kwa kupata kura 1,275, CUF 275, Chadema 57 na ADC 36.
Kata ya Mabanda, CCM 783, CUF 541, Chadema 27, ADC 66 na TLP kura tatu.
Kwa mujibu wa mmoja wa wasimamizi wa uchaguzi wa kata alisema kitendo
cha kukatika kwa umeme kimesababisha kuchelewa kwa matokeo katika
baadhi ya kata.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment