Mkutano wa kilele wa mameya na wabunge kuhusu hali ya hewa umefunguliwa
mjini Paris na rais Francois Hollande pembezoni mwa mkutano wa
mabadiliko ya tabia nchi mashuhuri kwa jina la COP21.
Mbali na rais Francois Hollande na meya wa jiji la Paris Anne
Hidalgo,mkutano huo wa kilele kuhusu hali ya hewa unahudhuriwa pia na
meya wa zamani wa jiji la New-York Michael Blomberg ambae pia ndie
mjumbe maalum wa Umoja wa Mataifa anaeshughulikia masuala ya miji na
mabadiliko ya tabianchi ,mcheza sinema wa kimarekani Robert Redford na
gavana wa zamani wa jimbo la California Arnold Schwarzenegger.
Wawakilishi wa mataifa 195 katika mkutano wa mabadiliko ya tabianchi
yanayojulikana kama COP21,wataendelea kwa upande wao na majadiliano yao
makali hadi decemba 11 ijayo lengo likiwa ni kufikia makubaliano ya
kupunguza hali ya ujoto katika sayari yetu.
Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki Moon,amerejea Paris akiwa na
matumaini mema ya kufanikiwa mazungumzo hao anasema:"Nimepata moyo kwa
kile nilichokiona na kukisikia katika ufunguzi wa CP21.Viongozi wa dunia
wamefanya kile wanachopaswa kukifanya-yaani kuyapa msukumo
majadiliano.Takriban nchi zote zimewasilisha mipango ya kimkakati
inayojulikana kama INDC(au michango inayodhamiriwa kutekelezwa kitaifa).
Mataifa mengi tajiri yametoa ahadi thabiti za kupunguza moshi wa sumu
na nchi nchi zilizoendelea zimetoa ahadi ziada kuzisaidia nchi maskini
na zile, zinazoweza kuathirika,kukabiliana na madhara ya mabadiliko ya
tabia nchi."
Mivutano imeanza kuchomoza kati ya nchji za kaskazini na zile za kusini.
Hata hivyo dalili za mivutano zimeanza kuchomoza; nchi zinazoinukia
zinaonyesha kukasirishwa na mkondo wa mazungumzo.Nchi hizo zimeyalaumu
mataifa tajiri kupuuza "hofu za nchi masikii zaidi na zinazoweza
kuathirika zaidi.
"Risala tunayopokea kutoka mataifa tajiri linapohusika suala la msaada
wa fedha ili kujiambatanisha na mabadiliko ya tabianchi ni "kwamba hamna
kitu" amesema mjumbe wa Bolivia Juan Hoffaister kwa niaba ya kundi la
mataifa 77 pamoja na China.
Mataifa yanayoinukia yanataka fedha bilioni 100 zilizoahidiwa hadi
ifikapo mwaka 2020 na mataifa ya kaskazini,zisisalie ahadi tupu na
zizidishwe pia baada ya muda huo na kwamba sehemu kubwa ya fedha hizo
zitumike katika kugharimia madhara ya mabadiliko ya tabia nchi.
Katika wakati ambapo wajumbe mkutanoni wanabidi wamkabidhi mwenyekiti wa
COP21,Laurent Fabius,mapendekezo yao hadi disemba tano mchana,mjumbe wa
Norway Aslak Brun ameukosoa ukosefu wa nia ya kuijongeza misimamo ya
kila upande.
Kwa vyovyote vile iwavyo, nitakabidhiwa mapendekezo yote saa sita
mchana."Amesema waziri wa mambo ya nchi za nje wa Ufaransa,ambae ndie
mwenyekiti wa mkutano wa mabadiliko ya tabianchi COP21.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment