Kutokana na hali hiyo, kocha wa Yanga, Hans van der Pluijm, ameanza
kusaka mbinu za kupata ushindi katika mechi zijazo za Ligi Kuu Tanzania
zitakazochezwa kwenye Uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga ambao mazingira
yake amedai si mazuri.
Yanga itashuka kwenye uwanja huo kuikabili African Sport na Mgambo JKT Desemba 12 na 16.
Akizungumza,Pluijm alisema kikosi chake
kinakuwa kwenye wakati mgumu kinapocheza nje ya Dar es Salaam, sababu
kubwa ikiwa ni ubovu wa viwanja vya mikoani.
"Tunakuwa na wakati mgumu sana tunapocheza nje ya Dar es Salaam, timu pia hukamia," Pluijm alisema.
"Tutacheza aina ya mpira utakaoendana na uwanja pamoja na wapinzani wetu, kikubwa tunataka ushindi bila kujali idadi ya magoli."
Kocha huyo alisema kuwa kutokana na changamoto hiyo, ameandaa
programu maalum ya mazoezi itakayoendana na uwanja huo ili kupata
matokeo mazuri katika mechi hizo mbili.
Katika mazoezi ya juzi na jana Pluijm, aliwasisitiza wachezaji wake
kucheza mpira wa pasi ndefu huku akiwataka kutumia kila nafasi ya
kufunga wanayoipata.
Katika hatua nyingine, wachezaji wa Yanga waliokuwa kwenye kikosi
cha timu Kilimanjaro Stars na Zanzibar Heroes zilizong'olewa mapema
kwenye michuano ya Kombe la Chalenji inayoendelea Ethiopia, wanatarajia
kujiunga na wenzao Jumamosi kuendelea na mazoezi ya timu hiyo
yanayofanyika kwenye Uwanja wa Boko Veteran.
Nyota wa Yanga walikokuwa kwenye vikosi hivyo ni Simon Msuva,
Kelvin Yondani, Deus Kaseke, Salum Telela na Malim Busungu (Kilimnajaro
Stars) pamoja na wale wa Zanzibar Heroes: Nadir Haroub 'Canavaro' na
Haji Mwinyi.
Kikosi hicho cha Yanga kitaondoka Dar es Salaam kwenda Tanga Desemba 7 tayari kwa michezo hiyo.
0 comments:
Post a Comment