Kikosi cha polisi nchini Burundi
kimeripoti kukamata silaha kadhaa za kivita zilizokuwa zimefichwa katika mtaa
mmoja wa mji mkuu wa Bujumbura.
Kikosi hicho cha polisi kilifanikiwa
kuzitia mikononi silaha hizo hapo jana wakati wa operesheni iliyofanyika katika
mtaa wa Ngagara.
Wakaazi wa mtaa huo walitoa taarifa
kwa polisi kuhusiana na maficho ya silaha hizo na kuwawezesha kuzikama kwa
urahisi.
Silaha hizo zilizokamatwa zilikuwa ni
bunduki 5 aina ya Kalashnikov, kombora 1, mabomu 29 pamoja na risasi nyingi.
Wakati huo huo, washukiwa wawili pia
walitiwa mbaroni baada ya kuhusishwa na umiliki wa silaha hizo.
Ngagara ni mojawapo ya mitaa
iliyofanya maandamano ya kupinga uongozi wa rais Nkurunziza kwa muhula wa tatu.
0 comments:
Post a Comment