Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr.John
Pombe Magufuli amekutana na kufanya mazungumzo juu ya hali ya siasa ya Zanzibar
na makamu wa kwanza wa rais wa serikali ya mapinduzi ya Zanzibar Maalim Seif
Sharifu Hamad Ikulu Jijini Dar es Salaam.
Viongozi hao wawili wamekutana na kufanya mazungumzo
hayo ikulu jijini Dar es Salaam kufuatia maombi ya Maalim Seif Sharif Hamad ya
kutaka kukutana na rais Dr.John Pombe Magufuli na kufurahishwa na hali ya
usalama na utulivu inayoendelea ambapo makamu huyo wa kwanza wa rais wa
Zanzibar amemueleza rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr.John Pombe
Magufuli juu ya hali ya siasa ya Zanzibar kadri anavyoifahamu yeye.
kwa upande wake rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dr.John Pombe Magufuli amemshukuru Maalim Seif Sharif Hamad kwa
taarifa kuhusiana na hali ya siasa Zanzibar na kumsihi waendelee na mazungumzo
hadi suluhisho muafaka lipatikane.
Aidha viongozi hao wawili wamewaomba wananchi
waendelee kuwa watulivu ili kutoa nafasi ya majadiliano yanayoendelea kufikia
hatma njema na kuelezea matumaini yao kuwa vyama vya CCM na CUF haviwezi
kushindwa kupata suluhu ya mgogoro huo.
0 comments:
Post a Comment