Baadhi ya waumini wa dini ya Kiislamu na
Kikristo nchini Kenya wameshambuliwa na kikundi cha Al Shabaab
wakati wakisafiri kwa basi kutoka mji mkuu wa nchi hiyo Nairobi kuelekea eneo
la Mandera.
Waumini hao walishambuliwa baada ya wapiganaji hao kulisimamisha basi na kuwataka wakae katika makundi mawili ya Wakristo na waislam ili waweze kuwaua wakristo kitendo ambacho kilipingwa na Waislamu ndipo shambulio hilo lilipotokea.
Katika tukio hilo ambalo limetokea eneo la Kaskazini Mashariki mwa Kenya karibu na mpaka na Somalia watu wawili waliuawa na wengine kujeruhiwa kufuatia kukaidi kwao kugawanyika kwa misingi ya dini.
Ikumbukwe kuwa mwezi april mwaka huu watu 148 waliawa kwenye chuo kikuu cha Garisa kufuatia shambulio la kigaidi lililofanywa na wapiganaji hao wa Al Shabaab.

0 comments:
Post a Comment