Uchaguzi wa wabunge na urais uliopangwa kufanyika
jumapili hii nchini haiti umeahirishwa,baraza la muda la uchaguzi limetangaza
katika taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa jumatatu hii usiku. hakuna
tarehe rasmi ambayo imetangazwa kufanyika kwa uchaguzi huu.
taarifa hii imekaribishwa na vyama vya wagombea
wawili wa urais, jovenel moïse na jude célestin, lakini upinzani bado unaomba
tume huru kuchunguza madai ya udanganyifu uligubika duru ya kwanza ya uchaguzi
wa urais.
kwa mujibu wa mwandishi wa rfi, katika mji wa
port-au-prince, amélie baron, tangazo la jumatatu hii usiku la baraza la muda
la uchaguzi (cep) la kuahirishwa kwa uchaguzi wa urais na wabunge
halikushangaza wengi. lilikuwa likisubiriwa na raia pamoja na vyama vya kiraia.
itafahamika kwamba mgombea wa upinzani, jude
célestin, alikuwa bado hajatamka hadharani hata neno moja tangu kuanza kwa
kampeni za uchaguzi. kuahirishwa kwa uchaguzi huo, kwa upande wake ni
"hatua nzuri katika mwelekeo sahihi", lakini amesema jumatatu usiku
kwamba alikuwa bado anasubiri "kuundwa kwa tume sahihi ya uchunguzi."
tume ya uchunguzi
jude célestin, mshirika wa karibu wa rais wa zamani
réne préval, hapa anaikaba moja kwa moja serikali iliopo madarakani, akikanusha
ufanisi wa tume iliyoundwa alhamisi iliyopita na michel martelly. tume ambayo
hata hivyo ni dhaifu kwa sababu mmoja wa wajumbe wake bado anazusha masuali
mengi kuhusu kazi anayopashwa kufanya.
katika kambi ya jovenel moïse, mgombea kwa tiketi ya
utawala, tangazo la kuahirishwa kwa uchaguzi limepokelewa vizuri. grégory
mayard paulo, mmoja wa wanasheria wa chama cha phtk chama, ametangaza kuwa
angeweza "kuheshimu uamuzi wowote unaochukuliwa na cep".
sasa muda unayoyoma kwa kukamilisha uchaguzi huu
nchini haiti kwani ufunguzi wa vikao vya bunge umepangwa januari 11 na rais
mtarajiwa anapaswa kuanza shughuli zake tarehe 7 februari.
0 comments:
Post a Comment