Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli amekutana na kufanya
mazungumzo na Spika wa seneti ya Burundi na mjumbe maalum wa rais wa
Jamhuri ya Burundi Reverien Ndikuriyo Ikulu Jijini Dar es Salaam juu ya hali
ilivyo nchini Burundi na jitihada zinazochukuliwa na tanzania ambayo ni
mwenyekiti wa jumuia ya Afrika mashariki ili kusaidia uwepo wa hali ya utulivu
nchini humo.
Kikao
hicho kilichohudhuriwa pia na waziri wa mambo ya nje Afrika Mashariki kikanda
na kimataifa balozi Augustine Mahiga kilicholenga kuzungumzia hali ya kisiasa
nchini Burundi,serikali ya Burundi imeihakikishia tanzania kuwa iko tayari
kufanya mazungumzo ya amani na wadau wote wa siasa nchini Burundi.
Balozi
mahiga ameongeza kuwa katika kikao hicho ujumbe huo umeelezea hatua ya bunge la
nchi ya Burundi kupinga uamuzi wa baraza la usalama la umoja wa afrika wa
kutaka kupeleka majeshi yake nchini Burundi kwa kuwa inaamini kuwa hakuna hali
ama dalili za kutokea kwa mauaji ya kimbari kama ya rwanda na kwamba kuna
utulivu nchini humo tofauti na wasiwasi wa umoja wa Afrika,jumuiya za kimataifa
hasa umoja wa ulaya,na kwa kiwango fulani umoja wa mataifa unaotoa msukumo wa
kutaka kuyapeleka majeshi ya kulinda amani nchini burundi.
Kuhusiana
na suala la bunge la Burundi kupinga kupelekwa kwa majeshi ya umoja wa afrika
nchini humo balozi Augustine Mahige amesema Rais Dr.John Pombe Magufuli ametoa
mapendekezo.
sambamba
na mapendekezo hayo rais magufuli amemuagiza balozi maiga kwenda nchini burundi
kutazama, kujiridhisha na kutathmini hali halisi ilivyo hususani katika suala
la amani hasa ulinzi na usalama wa raia si katika jiji la Bujumbura pekee bali
pia maeneo mengine ya nchi hiyo ili kufahamu sababu zinazowafanya warundi
kukimbia nchi yao na kukimbilia tanzania kama wakimbizi.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimkaribisha Ndugu Reverien Ndikuriyo Spika wa Seneti na Mjumbe Maalum wa Rais wa Jamhuri ya Burundi Ikulu jijini Dar es salaam Desemba 22,2015.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Ndugu Reverien Ndikuriyo Spika wa Seneti na Mjumbe Maalum wa Rais wa Jamhuri ya Burundi Ikulu jijini Dar es salaam Desemba 22,2015.
0 comments:
Post a Comment