Image
Image

TANESCO yanasa watu wanaojiunganishia umeme kinyemela Kijitonyama.

Shirika la Umeme Tanzania TANESCO Kanda ya Kinondoni Kaskazini  limeendelea na msako wa nyumba kwa nyumba eneo la  Kijitonyama Jijini Dar es Salaam na kufanikiwa kukamata watu wanaodaiwa kuhujumu  shirika hilo kwa kuharibu mita  kwa kuongeza nyaya kinyume cha sheria ili  watumie  umeme bila kupimwa k upitia   luku .
Tambarare halisi imeshuhudia maofisa  wa TANESCO  wakifungua na kuonesha jinsi watuhumiwa hao walivyo fanikiwa kukwepa gharama halisi  wanazotakiwa kulipa kwa matumizi yao .
Maa fisa hao wametaja majina ya baadhi  ya nyumba ambazo zimechukuliwa  hatua na TANESCO katika eneo la Kijitonyama baada ya kukutwa na hatia kuwa ni zil e zinazomilikiwa na DENIS MTUI,  ABDALA ALLY KESSY na JAMES MAPUNDA .
Kabla ya wafanyakazi wa TANESCO kubainisha hatua wanazotarajia kuchukua baada ya zaoezi hilo ,  baadhi ya wananchi  waliokutwa katika nyumba hizo  wamepewa ufafanuzi wa hujuma i liofanywa katika nyumba wanazoishi  na baadhi yao walioonesha kutofahamu kilichofanywa katika mita hizo.

Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment