Na Hemed
Kivuyo
Nilisoma
na mtu mmoja anaitwa Bakari kule Arusha, huyo jamaa alikuwa mjeuri sana na
msumbufu darasani. Mara nyingi tunapokuwa mstarini yeye hayupo hujificha
chooni. Tunapoingia darasani yeye huingia kwa dirishani au huingia kwa
kujificha akiwa mchafu asiyeweza kufua hata shati lake.
Mara
kadhaa alikuwa haandiki na akiulizwa hujibu kwakukaa kimya mpaka mwalimu
hutumia fimbo pamoja nahayo huwa ‘sugu’ tu.
Panapotokea
kelele darasani mwalimu anapoingia tu kuanza kumuangalia Bakari alipokaa na
kisha humwita mbele na kumuadhibu hata kama Bakari hakuwa mleta fujo kwa wakati
huo.
Siku
moja tulikuwa mstarini na Bakari alikuwepo, siku hiyo hata mimi nilishangaa
kwanini Bakari yupo mstarini tena alikuwa kafua nguo zake na zilionekana
kupigwa pasi alikuwa nadhifu ‘barobaro’.
Viatu
vilionekana kung’aa barabara huku akinukia manukato, hakika alikuwa Bakari
halisi tofauti na siku zote nilizomjua.
Wakati
tumeshakaguliwa na kuingia darasani, Bakari alikuwa wa mwisho kuingia darasani,
mwalimu mmoja hivi simkumbuki jina akamuona Bakari akiwa wa mwisho. Mwalimu
yule haraka alimwamuru Bakari ashike chini kisha akamnyuka ‘viboko’ vitatu vya
nguvu kisha akaanza kumtajia makosa yake.
Kwanza
alimwambia amechelewa na hakukaa mstarini na tatu alikuwa mchafu jambo ambalo
kwa siku hiyo halikuwa kweli. Bakari alikuwa msafi na aliwahi ila alikuwa wa
mwisho katika mstari na alipolala chini kuchapwa mwalimu hakuona mavazi yake
kuwa ni masafi.
Baada ya
kipigo kile mwalimu alipewa taarifa kuwa makosa yote aliyomsomea Bakari
hayakuwa sahihi alimuomba radhi ingawa Bakari alishapata maumivu.
Ndugu
zangu hiyo ni hadithi fupi na yakweli ambayo ninaifananisha na haya yanayotokea
kwa sasa baina ya msemaji wa Yanga Jerry Muro na msemaji wa Simba Haji Manara.
Binafsi
nilikuwepo siku ile Muro anaongea nasi (waandishi wa habari) aliongea
mengi ya klabu hiyo lakini pia alimshukia Haji Manara yeye mwenyewe akiita
‘kutumbua majipu’.
Kumekuwepo
na maneno kuwa Muro ametoa maneno yakibaguzi dhidi ya Hadji Manara lakini
maneno yenyewe hayatajwi ni yapi na ambayo mimi sikuyasikia siku hiyo.
Nilimsikia
Jerry akisema Haji amemtaja kuwa yeye ni mtu kutoka Kilimanjaro na hajui soka,
pia akaseka Yanga inapendelewa na Shirikisho la Soka nchini TFF, hayo ni kwa
mujibu wa Jerry.
Jery
akasema kwakuwa Haji alimtaja moja kwa moja katika chombo cha Habari kuwa yeye
hajui soka kwakuwa ametoka Kilimanjaro na yeye anamtaja na kumjibu kwa jina
lake kwakuwa mwiba hutokea pale ulipoingilia.
Kwa
mujibu wa Jery, Manara alimtaja kwa jina kuwa ametoka huko wasipojua soka.
Kama
tukiamua kuzama katika Kiswahili na kupata maana halisi ya ubaguzi, basi Haji
Manara na Jerry Muro wamebaguana wenyewe. Ukisikiliza kwa makini maneno ya Muro
utaona ametamka maneno yale kiufundi mkubwa, ametamka kwa mfumo wa kujibu.
Naamini
kabisa kama watapelekwa katika mahakama zetu zakiraia mfano Kisutu hakutokuwa
na ushahidi wa moja kwa moja wa kumkuta Jerry Muro na hatia.
Nasema
hivyo kwasababu Mahakama huhitaji ushahidi wa moja kwa moja na usiyokuwa na
shaka hata kidogo.
Jerry
ametoa shutuma hizo kwa ufundi mkubwa ambao haumuingizi hatiani labda kwa
kamati ‘zakisiasa’ lakini kisheria hawezi kukutwa na hatia.
Mfano
mimi nimelaumiwa na rafiki yangu Issa na akanitupia shutuma kali na maneno
yasovikwa nguo, nami nikamjibu na katika kumjibu nikamjibu kama ifuatavyo.
“Mimi
siwezi kutishwa na mtu hohehahe kama Issa, eti mtu anasema mimi sijasoma basi
aende kushtaki, sibabaishwi na paka anayehitaji hisani kupata mlo”, mwisho.
Tukienda
Mahakamani Issa kanishtaki mimi nimemuita yeye ni ‘Paka’ hawezi kushinda hiyo
kesi.
Hata
kama kuna ushahidi wa sauti na picha nikitamka maneno hayo kwasababu nyingi
zakisheria Issa hawezi kushinda kesi.
Hilo ni
suala moja, lakini suala la pili kama kweli Haji Manara alianza kutoa maneno
hayo yakibaguzi dhidi ya Muro hata kama hakusema katika chombo cha habari ni
dhambi katika soka. Ukiua mtu haijalishi ulimuua wapi msingi ni kwamba umeua.
Miaka
ile ya 1890 na kuendelea alikuwepo Mwanadada aliyeitwa Mtumwa, lakini jina lake
halisi ni Siti binti Saady. Alililewa katika mazingira ya wakati huo mwanamke
hapewi nafasi ya kwanza na kulijaa ubaguzi wa hali ya juu.
Alibaguliwa
na kulikuwa na ubaguzi wa rangi kutoka kwa jamii ya waarabu. Kulitokea uhasama
baina ya waarabu na weusi. Siti alikuwa mweusi. Siti alikuwa mwimbaji mzuri na
umma ulimpenda, alikuwa na sauti muruwa na kuwavuta wengi.
Katika
moja ya majibizano hayo, wabaya wa Siti wakamwambia Siti..‘Siti kawa mtu lini
kaja mjini na kaniki chini, kama si sauti angekula nini.
Siti
akawajibu kupitia wimbo wake akisema “hasara ya mtu kukosa akili”.
Kimsingi
ukiangalia vyema na kusikiliza vyema majibu ya Siti huwezi kumuhukumu moja kwa
moja kuwa aliwatusi wabaya wake.
Muro
kusema Haji akahangike na yake yanayomshinda siyo ubaguzi, kusema hana gari
siyo ubaguzi, kusema anaishi kwao siyo ubaguzi na kama kweli alisema hivyo.
Kuna
ukweli na kuna urongo. Kama ni kweli basini uhalisia hakuna unafiki hapo.
Yawezekana ni maneno ya kuudhi lakini siyo yakibaguzi na hapa najadili maneno
ya kibaguzi kwakuwa ndiyo Jerry analaumiwa nayo lakini naona ni maneno ya
kuudhi siyo kibaguzi.
Majibu
hayo makali pia hutegemea mtoa kauli wa awali aliyatoa kwa ukali kiasi gani.
Jery
alitumia lugha za kuudhi wakati akijibu mapigo kwa hasimu wake kisoka ingawa
hawapaswi kuwa mahasimu kama zilivyo timu zao.
Binafsi
siungi mkono mameno ‘machafu’ na yenye ubaguzi ndani yake miongoni mwa jamii
lakini lazima tuangalie haki ilipo kwakuwa haki huwa inanyooka.Haji Manara naye
ni mkosefu ila ni mkosefu anayelindwa na wengi na hapo ndipo anapoficha makucha
yake.
Shirikisho
la kandanda limetajwa na Haji Manara kuwa linaipendelea Yanga, shirikisho
halijakanusha wala halijamchukulia hatua Hadji Manara.
Bali
shirikisho limesherehesha kauli ya Manara kwakudhamiria kumchukulia hatua
msemaji wa timu wanayoipendelea, kwa mujibu wa Haji.
Kama
Jerry muro atakuwa na tuhuma za kutoa lugha zakibaguzi basi nitashangaa sana
kama tuhuma hizo hatokutwa nazo Haji Manara.
Haji
Manara mwenye sifa ya upole wa Twiga lakini mwenye maneno makali ambayo
yaliwahi kuwajeruhi hata waandishi wa Habari kwa kuwaita ni wenye ‘kuingiza
ndimi zao puani’.
Tutoe
hukumu za haki ingawa mara nyingi chini ya Juha hamna haki, tusimuhukumu Jery
kama Bakari aliyezoeleka kuvunja kanuni za shule lakini siyo alipopewa adhabu
hakuvunja kanuni hizo.
Wahukumiwe
kwa kutoa lugha za kuudhi kwakuwa hata Haji hayupo salama.
0752
250157 au 0655 250157
0 comments:
Post a Comment