Jopo la Watu Mashuhuri la Umoja wa Mataifa la Kupendekeza
Namna Bora ya Dunia Kukabiliana na Majanga ya Afya limekamilisha kazi yake wiki
iliyopita jijini New York. Jopo hilo linaloongozwa na Rais Mstaafu Jakaya
Mrisho Kikwete lilikabidhiwa jukumu hilo na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa,
Ban Ki moon tarehe 2 Aprili, 2015 na kupewa muda wa kuanzia Mei hadi Desemba
2015 kukamilisha kazi yake.
Jopo limefanya mikutano minne na kukutana na wadau mbalimbali wa afya zikiwemo taasisi za Umoja wa Mataifa, wadau wa maendeleo, wataalam mbalimbali na kupokea maoni na uzoefu kutoka kwa nchi zilizoathirika na ugonjwa wa Ebola.
Watu mashuhuri wanaounda Jopo hilo ni Mheshimiwa Michelin Calm-Roy aliyekuwa Raise wa Shirikisho la Uswisi; Mheshimiwa Marty Natelagawa aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje wa Indonesia; Mheshimiwa Joy Phumaphi, aliyekuwa Waziri wa Afya wa Botswana na Naibu Mkurugenzi Mkuu wa WHO, Mheshimiwa Celso Amorim aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje wa Brazil na Rajiv Shah aliyekuwa Mkuu wa Shirika la Misaada na Maendeleo la Marekani (USAID).
Jopo hilo linatarajia kuwasilisha ripoti yake kwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa mwezi January, 2016 na baadae kuwasilishwa kwenye Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa na Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa.

0 comments:
Post a Comment