Mashariki mwa DRC katika wiki za hivi karibuni kulishuhudiwa
ongezeko la machafuko ya kundi la waasi wa ADF. Kundi hili la waasi kutoka
Uganda lilifurushwa rasmi katika ardhi ya Uganda. Hata hivyo kuna uvumi kwamba
bado kundi hilo linaendesha harakati zake nchini Uganda.
Mjini Kampala, hawana shaka kwamba waasi wa ADF wanaendesha
harakati zao nje ya Uganda. Lakini wamekua wakijaribu kuvuka mpaka na kuendesha
machafuko nchini humo. Hayo yamefahamishwa na Waziri wa ulinzi wa Uganda Krispo
Kiyonga."Tunawasubiri mpakani iwapo wanakuja, wao ndio watakufa, si raia
wetu . "
Lakini karibu na mpaka wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo,
hali inaonekana kuwa tete. Ni vigumu kudhibiti hali ya mambo katika eneo la
Mpondwe. Katika milima ya Rwenzori, wafanyabiashara wanakabiliwa na visa vya
uporaji, utekaji nyara na mauaji. Luteni Nsamba anakubali kwamba si rahisi
kudhibiti hali ya usalama kwenye mpaka.
"Nataka kuwaonyesha jinsi kudhibiti mipaka barani
Afrika ni vigumu ikilinganishwa kwa mfano na mipaka ya Ukraine au Ubelgiji.
Katika nchi hizo, wakati kunaonekana tatizo la wakimbizi, kwa mfano, nchi hizi
zinaharakia moja kwa moja kuweka vizuizi. Kwa hiyo mipaka na usimamizi kwenye
mipaka hiyo vinakwenda sambamba na teknolojia", amesema Kanali Nsamba.
Hata hivyo wakazi wa kijiji cha Kichwamba nchini Uganda,
wanasema wanatiwa hofu na hali ya usalama ambayo inaendelea kudorora siku baada
ya siku. Mkazi mmoja wa kijiji hicho amesema kuna uvumi kwamba waasi wa ADF
bado wapo nchini Uganda. "Ni rahisi. Wanaweza kujifananisha na raia wa
kawaida. Si rahisi kuwatambua."
Kirasmi, waasi wa ADF wako upande wa Jamhuri ya Kidemokrasia
ya Congo. Vyombo vya habari nchini Congo vimearifu kwamba waasi hao walionekana
hivi karibuni upande wa Ntoroko.
0 comments:
Post a Comment