Katika
kuhakikisha kuwa tofauti kati ya wakulima na wafugaji nchini ambazo zimekuwa
kwa muda mrefu zikisababisha machafuko zinakwisha na kubakia historia,waziri wa
kilimo, ufugaji na uvuvi Mh.Mwigulu Nchemba amefika Mkoani Kagera,kutatua kero
za wafugaji na wakulima hao.
Waziri
Nchemba ambaye amelivalia njuga suala hilo na kutaka kuhakikisha kuwa mapigano
kati ya wakulima na wafugaji hayajitokezi amelazimika kuongozana na Naibu
waziri wa Mali Asili Mh.Ramo kwa lengo la kusaidia kuanzisha utaratibu wa
kuyapitia upya mapori ya akiba ya Maswa,Kimisi,Burigi suluhisho la kudumu na
pia kuhakikisha kuwa suwala la malisho kwa wafugaji linapata utatuzi wenye
tija.
Pia
Waziri Nchemba ametoa rai kwa wafugaji na wakulima wote kulinda maeneo ya
hifadhi yaliyotengwa,Kama dhamira ya Rais John Pombe Magufuli ilivyojitoa
kuhakikisha changamoto hizo zinakwisha.
Amewahakikishia
wafugaji na wakulima kwamba Wizara yake kwa wakulima,Wafugaji na Wavuvi
itahakikisha kuwa inamaliza na kutatua kero zao kwa kuzipatia majawabu ya
kudumu hatua kwa hatua.
0 comments:
Post a Comment