Baada ya kutokea kwa mapigano ya wenyewe kwa wenyewe katika jimbo la
Biafra nchini Nigeria yaliyosababisha vifo vya watu milioni moja,
vuguvugu kusini mashariki mwa nchi hiyo linataka jimbo la Biafra
lijitawale.
Miito kama hii imekuwa ya mara kwa mara tangu kiongozi wa kundi hilo
ambalo Ikedi anawakilisha katika eneo la Enugu ulio mji mkuu wa eneo
hilo alipokamatwa mwezi Octoba,na kusababisha maelfu ya watu katika eneo
linalozalisha mafuta kwa wingi la kusini Mashariki kujiunga na
maandamano hayo katika wiki za hivi karibuni wakitaka aachiliwe huru.
Hii ni changamoto nyingine kwa Rais Muhammadu Buhari ambaye anakabiliana
na kushuka kwa uchumi katika taifa hilo ,kundi la itikadi kali la Boko
Haram kaskazini mashariki na hofu ya kurejea kwa shughuli za kijeshi
katika eneo tajiri kwa mafuta la Delta Kusini wakati muda wa mwisho
utakapomalizika mwezi Disemba.
Kama ilivyo kwa wengi katika vuguvugu la wanaotaka kujitenga katika eneo
la kusini mashariki,Ikedi alizaliwa muda murefu baada ya kumalizika kwa
vita vya Biafra.
Bila kuwa na chochote kitakachoashiria anaunga mkono kujitenga kwa
Biafra kama vile bendera au fulana,ili kuepuka kuwavutia polisi, amesema
umaskini na kiwango cha juu cha ukosefu wa ajira katika eneo hilo ni
ishara ya kutelekezwa na serikali.
"Wanataka kutufanya masikini .Wanaamini njia ya pekee kututawala ni
kuendelelea kututaabisha"Ikedi amesema kwa sauti ya kutetemeka huku
akisema kundi lake la watu asili wa Biafra (IPOB) wanataka kura ya
maoni.
Wanalalamika eneo lao limetelekezwa
Kundi hilo linaelezea matatizo yanayowafanya watake jimbo la Biafra liwe
huru, swala ambalo msemaji wa rais Buhari, Garba Shehu alikataa
kuzungumzia akiongeza kuwa hana ufahamu kuwa serikali inafanya chochote
kuhusu swala hilo.
Barabara kuu zinazounganisha miji ya kusini mashariki zinavunja moyo
wafanyabiashara katika eneo hilo ambao wanasema barabara hizo ambazo
hazijawekwa lami kikamilifu,zina mashimo, zinastahili kuwa kichocheo cha
biashara lakini sasa ni hatari kuzitumia.
Taka iliyopembeni mwa barabara,pamoja na harufu mbaya kutoka kwa mfumo
wa maji machafu usiofunikwa inaelezea kutengwa kwa miaka 45 tangu
kumalizika kwa vita vya wenyewe kwa wenyewe.
Mapigano ya 1967-70 yalifuatwa na jaribio la kujitenga la watu wa Igbo
mashariki.Wengi wa watu milioni moja walipoteza maisha yao kutokana na
njaa na maradhi na wala si vita.
Kama wakati huo kwa sasa,Watu wa Igbo wanasema wametengwa kutoka
nyadhifa za serikali na kunyimwa ufadhili muhimu wa kustawisha
muundombinu,shule na hospitali.
Kiongozi wa jamii ya watu wa Igbo wa Biafra Nnamdi Kanu mwanaharakati
ambaye anatumia muda wake huko Uingereza na Nigeria kwa kueneza mawazo
yake kwenye mitandao ya kijamii na Radio Biafra alikamatwa mwezi
uliopita kwa mashtaka ya uhalifu na kwa kuwa mwanachama wa kundi lisilo
halali.
Mchambuzi wa maswala ya kisiasa Oreke Chukwunolye amesema uamuzi wa
kumkamata Kanu,ambaye hakuwa maarufu ingawa ufuasi wake kwenye mtandao
wa kijamii unashinda uugwaji wake mkono sehemu za mashinani,ni kosa
kwani kukamatwa kwake kunamuongezea umaarufu na kumfanya atambulike
zaidi.
Bado kungali hali ya taharuki.Wanaoendeleza kampeni za IPOB wanasema
wamejitolea kufanya maandamano ya amani,lakini maandamano yao
yalisababisha jeshi la nchi hiyo kutoa onyo kwamba juhudi zozote za
kugawanya nchi hiyo,zitapingwa vikali.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment