Kwa zaidi ya miaka kumi sasa wafanyabiashara katika
soko la nyama mkjini Tabora wamekuwa wakitoa huduma za kitoweo hicho katika
mazingira magumu kutokana na kutokuwepo na kuharibika kwa Mwandao wa maji,huku
wakiingia gharama kubwa kununua maji,katika kile walichodai kuwa,manispaa ya
Tabora imewatelekeza,wakati wakilipa ushuru.
Wakizungumza na mara baada ya kulipiwa zaidi ya
shilingi laki nane,na mbunge wa jimbo la Tabora mjini Bw,Emmanuel Mwakasaka,
kwa ajili ya kurejesha huduma hiyo,wafanyabiashara wahao wamesema
kuwa, biashara ya nyama inahitaji usafi kwa lengo la kutoa huduma safi
na inayomvutia mlaji, na hivyo wamekuwa wakiingia gharama kubwa, ili
kukidhi haja hiyo.
Akitoa shukrani kwa niaba
ya wafanyabiashara hao,mwenyekiti wa soko hilo Bw.Ahamad Juma
amesema kuwa, kwa ujumla soko kuu la mjini tabora limekuwa likikabioliwa
na changamoto mbali mbali zikiwemo za uchakavu wa miundombinu na hivyo msaada
huo umefika kwa wakati muafaka, huku mwakilishi wa mbunge huyo Bw,Mussa Mdaki
akidai kuwa hatua inayofuata ni kurejesha umeme katikasoko hilo.
0 comments:
Post a Comment