Jeshi la polisi limewabaini wahamiaji haramu saba
wanaodaiwa kutokea nchini Ethiopia wakiwa wametelekezwa kwenye gari maeneo ya
Mikumi wilayani,kilosa mkoani morogoro,baadhi yao wakiwa wamepoteza maisha na
wengine hali zao zikiwa ni mbaya.
Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake
kamanda wa polisi mkoa wa Morogoro Leonarld Paulo amesema walifanikiwa kupata
taarifa kutoka kwa raia wema kuhusiana na uwepo wa wahamiaji hao haramu eneo la mikumi,ambapo baada ya kufika
walikuta wahamiaji haramu wanne wakiwa tayari wamefariki dunia huku wengine wawili
hali zao zikiwa ni mbaya na mmoja akiwa mzima
ambapo baada ya kuwahoji walidai kutokea
nchini ethiopia na walikua wakielekea
Afrika Kusini kwaajili ya kujitafutia maisha.
Katika hatua nyingine polisi wanamshikilia mtu mmoja
saidi mwinshee (32 ) mkazi wa kungwe tarafa ya Mkuyuni katika wilaya ya
Morogoro,akituhumiwa kumkatakata kwa panga hadi kufa mamayake mzazi sikudhani
mgumba mwenye umri wa miaka 70 na mkazi wa kungwe kwamadai ya kula chakula
chake ampapo uchunguzi wa awali wa polisi umebaini kijana huyo kuwa na matatizo
ya akili.
Kwa upande mwingine jeshi la polisi mkoani hapa
limetoa onyo kali kwa watu wanaojihusisha na usafirishaji wa wahamiaji haramu
nakuahidi kuwafuatilia na kuwakamata kwa hatua zaidi za kisheria,huku amanda
paul akiwataka wananchi wa Morogoro kusherehekea mwaka mpya kwa amani na
utulivu na ulinzi umeimarishwa katika maeneo mbalimbali kukabiliana na uhalifu
wowote utakaoweza kujitokeza.
0 comments:
Post a Comment