Baadhi ya vyama vya ushirika wa zao la korosho Mkoani Mtwara kikiwemo Chama Kikuu cha Ushirika cha Masasi na Mtwara MAMCU, vimefanikiwa kuwalipa wakulima kiasi cha zaidi ya shilingi bilioni 12.
Hiyo ni kwa ajili ya malipo ya kwanza na ya pili na bonasi kwa kipindi hiki cha ununizi wa korosho ukiendelea na kufuatia mafanikio hayo wakulima wameshauriwa kuacha kuuza korosho nje ya mfumo wa stakabadhi ghalani ili waweze kunufaika na kuipatia pia serikali mapato
Changamoto hiyo imetolewa na Kaimu Meneja Mkuu wa MAMCU Bwana KELVIN RAJABU na Katibu Mkuu wa Chama cha Msingi cha Kilimanjaro Bwana SAIDI HAMISI.
Licha ya kuwapo kwa mavuno machache ya korosho msimu huu kutokana na mvua chache ushindani wa minada ni mkubwa na wakulima wameweza kulipwa vizuri ukilinganisha na msimu wa mwaka jana.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment