Image
Image

Yanga yanyoosha mikono kwa Coutinho.


HATIMA ya kiungo wa Yanga Mbrazil Andrey Coutinho kuwemo katika kikosi hicho tayari imeamriwa na uongozi wa klabu hiyo, ambapo kwa sasa anatafutiwa timu au kuvunja mkataba wake.

Coutinho baada ya kurejea Dar es Salaam mwishoni mwa wiki iliyopita, akitokea kwao Brazil kwa mapumziko mafupi, ambapo jana klabu hiyo ilikuwa na kikao kujadili mustakabali wake ndani ya timu hiyo na kuamua kuachana naye.

Habari zilizopatikana Dar es Salaam jana kutoka kwa mmoja wa viongozi wa klabu hiyo, zinadai kuwa, kutokana na mchezaji huyo kutopata nafasi kwa Kocha Mkuu wa timu hiyo, Hans de Pluijm, hawaoni sababu ya kuendelea na mchezaji huyo.

Coutinho analipwa na klabu hiyo mshahara wa dola 3,000 za Marekani kwa mwezi (zaidi ya sh.milioni 6 za Tanzania).

„Kama klabu inalipa kiasi chote hicho cha fedha kwa mwezi kwa mchezaji huyo lakini hachezi, haina sababu ya kuendelea naye, tunajua ni kipenzi cha mashabiki lakini hatuna jinsi kwa hilo,” kilidao chanzo hicho.

Pia kuna taarifa kwamba klabu kadhaa ikiwemo za St George ya Ethiopia zinamtaka mchezaji huyo, hivyo Yanga ipo tayari kumuacha kwa sasa.

Lakini Yanga kwa sasa inafanya mchakato huo, kama pande mbili zitashindwa kufikia mwafaka, basi raia huyo wa Brazil ataendelea kubaki Yangahadimkatabawake utakapokwisha.

Coutinho alisajiliwa Yanga msimu uliopita chini ya kocha Mbrazil mwenzake, Marcio Maximo na hadi sasa ameichezea klabu hiyo mechi 36 na kuifungia mabao saba.

Alikuja nchini pamoja na mshambuliaji mwingine, Mbrazil Genilson Santana Santos ëJajaí ambaye aliachwa baada ya nusu msimu akiwa amecheza mechi 11 na kufunga mabao matano.

Wachezaji saba wa kigeni wanaokidhi kanuni ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania katika kikosi cha Yanga kwa sasa ni mabeki Mbuyu Twite (DRC), Vincent Bossou (Togo), viungo Haruna Niyonzima (Rwanda), Thabani Kamusoko (Zimbabwe), Coutinho (Brazil) na washambuliaji Amisi Tambwe (Burundi) na Donald Ngoma (Zimbabwe). 
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment