MCHEZAJI Brian Majwega raia wa Uganda sasa yupo huru kucheza Simba
katika Ligi Kuu bara.
Kwa takriban wiki mbili sasa kumekuwa na mgogoro
kati ya Simba na Azam FC kuhusu mchezaji huyo aliyesajiliwa na Azam
mwanzoni mwa mwaka huu.
Mgogoro huo ulitokana na mchezaji huyo kufanya mazoezi Simba, jambo
lililokuwa likipingwa na Azam kwa vile bado ilikuwa na mkataba naye.
Akizungumza Dar es Salaam msemaji wa Simba, Haji Manara alisema
wamefikia makubaliano maalumu na Azam na sasa Majwega ni mali yao.
“Majwega sasa rasmi Simba ni mchezaji wetu na tutamtumia kwenye ligi,
tumefikia makubaliano maalumu na Azam jana jioni (juzi),” alisema
Manara. Hata hivyo, si Simba wala Azam waliokuwa tayari kuzungumzia kwa
kina aina ya makubaliano waliyoafikiana.
Kabla ya kurejea nchini Majwega alirudi kwao Uganda baada ya kuona
hapati nafasi Azam, lakini pia alishindwa kucheza na kuamua kurudi
nchini. Baada ya kurudi Majwega aliandika barua Simba akiomba kufanya
mazoezi ili kulinda kiwango chake kwani hakuwa kwenye maelewano na klabu
ya Azam.
Majwega alirejea nchini na kuomba kufanya mazoezi na Simba ili
kulinda kiwango chake na ndipo Azam walipokuja juu kwamba hawatendewi
haki na Simba. Hii si mara ya kwanza kwa klabu hizo, ambazo inaaminika
ni marafiki kuingia kwenye mgogoro wa wachezaji.
Ilishawahi kuingia kwenye mgogoro wa kumgombea Shomari Kapombe na Ramadhani Singano, ambao kwa sasa wanacheza Azam FC.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment