Waziri wa Fedha nchini Dkt. Philip Mpango amesema
tayari Benki Kuu ya Tanzania (BOT) imeandikia barua benki ya Stanbic ya kusudio
la kuitoza faini ya shilingi bilioni 3, baada kugundua matatizo yaliyohusiana
na hasara itokanayo na mikopo katika Benk.
Dkt. Mpango amesema hayo leo Jijini Dar es Salaam
wakati alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kwa lengo la kutoa taarifa
kwa wananchi, kuhusu hatua ambazo zimechukuliwa dhidi ya benki ya Stanbic
Tanzania Limited kuhusana na ushiriki wake kuwezesha mkopo wa serikali wa dola
za Marekani milioni 600..
Aidha Dkt. Mpango amesema benki kuu imechukua hatua
hizo kama onyo kwa benki ya stanbic na ili iweze kuwa makini katika kuhakikisha
kuwa shughuli zake zinaendeshwa kwa mujibu wa taratibu za kibenki na kuzingatia
sheria.
Dkt. Mpango ameongeza kuwa hatua hiyo ni onyo kwa
mabenki na taasisi za fedha zisijihushishe na makosa ya ya aina hiyo ambayo ni
kinyume cha taratibu za kibenki na ni uvunjaji wa sheria za nchi.
0 comments:
Post a Comment