Bodi ya kudhibiti video na filamu nchini Kenya
(KFCB) imepinga hatua ya kampuni ya Netflix kuanza kutoa huduma zake nchini
Kenya.
Bodi hiyo imesema Netflix, kampuni inayouza video na
filamu kupitia mtandao, ni lazima ipate kibali cha kuhudumu nchini Kenya kabla
ya kuanza kutoa huduma.
Mwenyekiti wa bodi hiyo Askofu Jackson Kosgei
amesema video za Netflix hazijachunguzwa na kuorodheshwa kwa mujibu wa viwango
vya filamu vya Kenya.
Amesema katika baadhi ya video walizotazama, ingawa
hakuzitaja, zilikuwa zimeorodheshwa kwamba zinafaa kwa watoto wa umri wa miaka
13 lakini baada yao kuzitazama wakabaini zina picha za uchi, zinatumia lugha
chafu na zinatukuza matumizi ya dawa za kulevya.
“Tuna wajibu wa kuwalinda watoto na vijana
wasionyeshwe picha na video zinazoonyesha matukio ya vurugu na ukatili na
zinazochochea uchi na kushiriki ngono,” amesema Askofu Kosgei.
Bodi hiyo pia imesema katika mazingira ya sasa
ambapo ugaidi umekuwa tatizo kuu, serikali ina haki ya kufuatilia video ambazo
watoto na vijana wanatazama wasije kukumbatia itikadi kali.
Hatua ya bodi hiyo inaonekana kuenda kinyume na
ushauri wa waziri wa habari na mawasiliano Bw Joe Mucheru ambaye wiki iliyopita
alinukuliwa na gazeti la Daily Nation akishauri idara za serikali kusubiri mwongozo
kutoka kwa serikali.
Mamlaka ya Mawasiliano ya Kenya nayo pia ilikuwa
imesema Netflix haiwezi kudhibitiwa chini ya sheria za utangazaji Kenya.
0 comments:
Post a Comment