Image
Image

Chipsi kwa wajawazito chanzo cha maradhi ya kisukari.



Imeelezwa kwamba ulaji wa mara kwa mara wa viazi,bila kujali kama ni vya kuchemshwa au vya kukaangwa ama chips,unaweza kuongeza uwezekano wa mwanamke kuwa katika hatari ya kupata maradhi ya kisukari wakati wa ujauzito,wameeleza watafiti wa Marekani.
Hii labda ni kwa sababu wanga uliomo katika viazi unaweza kusababisha kuongezeka kwa viwango vya sukari zaidi, wanasema watafiti hao
Ulaji wa mara kwa mara wa viazi, bila kujali kama ni vya kuchemshwa au vya kukaangwa ama chips, unaweza kuongeza uwezekano wa mwanamke kuwa katika hatari ya kupata maradhi ya kisukari wakati wa ujauzito, wameeleza watafiti wa Marekani.
Aidha,kubadilisha ulaji huu wa viazi (chips) kwa wiki kwa kula mboga mboga nyingine kunaweza kuzuia hatari hii, wanaeleza waandishi wa utafiti huu.
Wataalam wa masuala ya lishe nchini Uingereza wanasema vyakula vyenye wanga ama vya kuongeza nguvu na joto mwilini kama vile viazi, vinapaswa kuwa theluthi moja ya vyakula vinavyoliwa na watu.
Utafiti huo unatarajia kuchunguza nini chanzo cha maradhi ya kisukari yanayowapata baadhi ya wanawake wawapo wajawazito .
Utafiti huu umefuatia wauguzi wawili waliopata ujauzito kati ya mwaka 1991 na 2001. Hakuna hata mmoja wao aliyewahi kuwa na maradhi ya kudumu kabla ya ujauzito.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment