Kesi ya kupinga bomoa bomoa iliyofunguliwa na mbunge
wa Kinondoni Maulid Mtulia(CUF) katika mahakama kuu kitengo cha cha Ardhi
inaanza kusikilizwa leo.
Kesi hiyo namba 822 ya mwaka 2015 ambayo imepangiwa
jaji Penterine Kente huku upande wa walalamikaji wakisimamiwa na wakili
Abubakar Salim.
Akizungumza na waandishi wa habari Mtulia amesema
kuwa katika kesi hiyo wawakilishi nane watawakilisha wananchi wa maeneo hayo.
Mbunge huyo alisema kuwa lengo si kufungua kesi hiyo
kupinga ubomoaji wa wakazi wa mabondeni bali anahitaji wananchi hao watendewe
haki ikiwa ni pamoja na kupewa viwanja walivyo ahidiwa.
Alisema wameamua kufungua kesi hiyo baada ya
kufuatilia suala hilo sehemu mbalimbali iliwa ni pamoja na Ofisi ya mkuu wa
Mkoa,Wilaya lakini hakuridhishwa na majibu ya viongozi hao.
“Maeneo mengine ya uongozi niliyokwenda najibiwa
kuwa viwanja walivyopewa baadhi na wengine kuahidiwa ilitokana na huruma ya
Rais mstaafu Jakaya Mrisho Kikwete”Alisema.
Hata hivyo bomoabomoa katika maeneo ya mabondeni
itazikumba nyumba zaidi ya 5000 kati ya hizo 114 tu ndizo zilizofanyiwa
tathmini.
Bomoabomoa hiyo inaendelea jijini ambapo mwishoni
mwa wiki waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo na makazi,William Lukuvi
alitembelea maeneo hayo ambayo yanapaswa kuendelea kubomolewa tena kuanzia leo.
0 comments:
Post a Comment