Watu wanne wameuawa na wengine 35 wamejeruhiwa baada
ya basi kampuni ya LUWINZO linalofanya safari zake kati ya Njombe na Dar es
Salaam waliolokuwa wakisafiria kugonga lori lililokuwa limeegeshwa pembeni mwa
barabara Mufindi mkoani Njombe.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Njombe Bwana PETER
KAKAMBA amesema kuwa ajali hiyo ilitokea eneo la Kinegembasi wilayani
Mufundi ambapo watu wawili waliofariki ni watumishi wa Basi la Luwinzo
huku akisema kuwa majeruhi hali zao zinaendelea vizuri.
Amesema kuwa majeruhi wa ajali hiyo 33 wamepelekwa
katika hospitali ya Mafinga na wawili wamepelekwa katika hospitali ya makambako
kwa matibabu zaidi.
Kamanda Kakamba amesema kuwa dereva wa Basi la
Luwinzo nimajeruhi na wanamshikilia dereva wa Lori kwa kupaki barabarani vibaya
na kusababisha ajali.
Like Page yetu
na uwe wa kwanza kupata habari.
0 comments:
Post a Comment