Watu wanane wakiwemo wanne wa familia moja
wamefariki dunia baada ya gari waliokuwa wakisafiria kutoka mkoani Geita
kuelekea jijini Dar es Salaam kusombwa na maji ya mafuriko katika eneo la
Bwawani wilayani Kongwa barabara kuu ya Dodoma Morogoro kufuatia mvua za masika
zinazoendelea kunyesha maeneo mbalimbali nchini.
Kwa mujibu wa kamanda wa Polisi mkoa wa Dodoma David
Misime amesema kuwa jeshi hilo lilipokea taarifa ya kujaa maji katika eneo hilo
na kisha kupeleka askari ambapo waliambiwa na baadhi ya wananchi waliokuwepo
eneo hilo kuwa kuna gari inaonekana ikielea kwenye maji
Jeshi hilo baada ya kupata taarifa hiyo lilifuatilia
na kubaini uwepo wa gari aina ya Toyota RAV 4 lenye namba za usajili T 516 DEP
mali ya Gerald riyoba ambaye ni msaidizi wa mkuu wa Jeshi la Polisi IGP Ernest
Mangu aliyefariki yeye mke wake na watoto wawili pamoja na Koplo Ramadhani
alikuwa Dereva wa gari hilo na msichana aliyetambulika kwa jina la Sara
anayedaiwa kuwa mfanyakazi wa ndani wa familia hiyo.
Kamanda Misime pia akabainisha katika zoezi la
kutafuta miili ya watu waliokuwemo kwenye gari hilo wakabaini pia kuwepo kwa
miili mingine miwili ambayo mmoja alitambulika kwa jina moja la Ludege afisa
mifugo wa kata ya pandambili wilayani kongwa huku mtu mwingine akishindwa
kutambulika
0 comments:
Post a Comment