Kesi ya uhujumu uchumi inayowakabili vigogo wa
Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) wanaotuhumiwa kuhusika na upotevu wa makontena
329 na ukwepaji wa kodi ya Sh. bilioni 12.7, imepigwa kalenda hadi Januari 27,
mwaka huu.
Kesi hiyo ilisogezwa mbele jana na Mahakama ya
Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam kutokana na kutokamilika kwa
upelelezi.
Akitoa uamuzi huo, Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi,
alisema mshitakiwa namba sita Harun Mpande bado ataendelea kuwa rumande
kutokana na kutotimiza masharti ya dhamana.
Washitakiwa wengine wanaokabiliwana kesi hiyo
ni aliyekuwa Kamishna wa Forodha na Ushuru wa TRA, Tiagi Masamaki ,Meneja wa
Kitengo cha Huduma za Ushuru, Habibu Mponezya, Bulton Kaisi na Msimamizi Mkuu
wa Bandari Kavu ya Azam-ICD, Eliachi Mrema.
Wengine ni, Mchambuzi Mwandamizi wa Masuala ya
Biashara TRA, Khamis Omar, Ofisa wa Kitengo cha Mawasiliano ya Kompyuta (ICT)
TRA, Haroun Mpande, Raymond Louis na Ashraf Khan.
Washitakiwa hao wanadaiwa kuwa, kati ya Juni Mosi na
Novemba 17, mwaka huu, siku isiyofahamika, walikula njama ya kutenda kosa la
kuidanganya serikali kwamba makontena 324 yaliyokuwa katika bandari kavu ya
Azam yametolewa baada ya kulipiwa kodi, huku wakijua siyo kweli.
0 comments:
Post a Comment