Mahakama kuu kanda ya Shinyanga imetengua pingamizi
lililokuwa limewasilishwa na wakili anayemtetea Bw.Jumanne Kishimba ambaye ni
mlalamikiwa katika kesi ya uchaguzi mkuu katika jimbo la Kahama mjini pingamizi
lililokuwa linaitaka mahakama kuondoa kipengele cha nane katika hati ya
mlalamikaji James Lembeli aliyekuwa mgombea ubunge kwa tiketi ya Chadema
kipengele ambacho kinalalamikia matumizi ya rushwa katika uchaguzi huo kwa
madai kuwa kipengele hicho kina mapungufu na hakikukidhi vigezo vya kisheria.
Kabla ya kusoma hukumu ya pingamizi hilo jaji
anayesikiliza kesi hiyo Bi.Victoria Makani ameeleza kuwa mahakama imesikiliza
maelezo ya pande zote mbili kwa umakini na kupitia vifungu mbalimbali vya
kisheria na kuona kwamba katika kifungu cha nane chenye vipengele vidogo A,B,C
na D kinacholalamikiwa kuwa kiondolewe hakuna sababu za msingi za kukiondoa ila
kinachohitajika ni ushahidi ambao utaionyesha mahakama ukweli wa madai ya
mlalamikaji.
Aidha jaji Victoria Makani baada ya kuyaeleza hayo
amesema kwa kuzingatia kanuni sheria na taratibu za Mahakama anamtaka
mlalamikaji ambaye ni Bw.James Lembeli kuwasilisha mbele ya mahakama ushahidi
wa tarehe ambayo tukio la vitendo vya rushwa lilifanyika,mahali na watu
waliopokea rushwa hiyo ndani ya siku saba na kuitaja tarehe kumi na nane ya
mwezi huu kuwa kesi itaendelea kusikilizwa.
0 comments:
Post a Comment