Wapalestina wanne wameuawa kwa kupigwa risasi baada
ya kujaribu kuwadunga visu wanajeshi wa Israel katika visa viwili tofauti,
jeshi la Israel limesema.
Visa hivyo vilitokea eneo la Ukingo wa Magharibi.
Watatu waliuawa katika makutano ya barabara ya Gush
Etzion, ambako visa kama hivyo vimewahi kutokea awali. Wa nne aliuawa karibu na
Hebron, jeshi limesema.
Hakuna mwanajeshi aliyejeruhiwa.
Maafisa wa afya wa Palestina wamethibitisha vifo
hivyo.
Vyombo vya habari Palestina vimetaja watatu hao kuwa
Muhanad Kawazbeh, 20, Ahmed Kawazbeh, 21, na Alaa Kawazbeh, 20, wote kutoka
kiji cha Sair, kaskazini mashariki mwa Hebron.
Wa nne ni Khalil Shalalda, 16, pia kutoka Sair.
Kumekuwa na ongezeko la visa vya mashambulio kati ya
Waisraeli na Wapalestina miezi ya hivi karibuni.
Waisraeli 22 na Wapalestina zaidi ya 140 wameuawa
tangu 1 Oktoba.
Waisraeli hao wameuawa kwa kudungwa visu, kupigwa
risasi na kugongewa magari.
Nusu ya Wapalestina waliouawa wamedaiwa na Israel
kuwa washambuliaji. Wengine wameuawa kwenye makabiliano na maafisa wa usalama.
0 comments:
Post a Comment