Waziri wa afya,maendeleo ya
jamii,jinsia wazee na watoto Mh.Ummy Mwalimu ameyasema hayo jijini Dar es Salaam
ambapo amesema familia zenye watoto wenye mahitaji maalum halikadhalika
zihakikishe zinawapeleka watoto hao shule ili kutoa haki sawa ya elimu.
Kuhusu suala la watoto wanaoomba
mitaani,wanaoishi katika mazingira hatarishi na walioajiriwa wakiwa na umri wa
kwenda shule mh mwalimu amesema.
Pia viongozi na watendaji wa mikoa na halmashauri, maafisa Maendeleo ya jamii na watendaji wa kata wameaswa kusimamia na kutekeleza
majukumu yao kwa kuhakikisha wanahamasisha jamii ipasavyo juu ya watoto
kujiunga na darasa la kwanza na kidato cha kwanza kwa mwaka huu.
Ummy amesema kuwa maafisa wa maendeleo ya jamii za mikoa,Halmashauri na kata zote hapa nchini watoe taarifa za utekelezaji wa jambo la watoto kwenda shule mwishoni mwa mwezi Februari mwaka huu.
Aidha Serikali inatoa rai kwa wazazi na walezi kuhakikisha kuwa watoto wote wanaendelea na masomo ya shule ya Msingi na Sekondari vizuri na wahudhurie masomo yao kwa ufanisi, pia serikali haitegemei kuona utoro wa watoto mashuleni kutokana na sababu zinazoweza kuepukika.

0 comments:
Post a Comment