Kwenye michuano ya Kombe la Mapinduzi kwa mwaka 2016
klabu ya Dar Es Salaam Young African ilishuka dimbani jana kucheza mchezo wa
nusu fainali ya pili dhidi ya klabu ya URA ya Uganda katika dimba la Amaan,
mchezo ambao ulikuwa unamtafuta bingwa mmoja kati ya timu hizo kwenda kucheza
dhidi ya Mtibwa Sugar katika hatua ya fainali ya michuano hiyo.
Yanga ambayo ilikuwa inaongoza katika msimamo wa
Kundi A ilianza kwa kupachika goli la uongozi dakika ya 13 kupitia kwa Amissi
Tambwe ambaye aliutumia vyema mpira uliopigwa kichwa na Simon Msuva na
kushindwa kutinga nyavuni, kipindi cha pili URAwaliendelea kuwa na nidhamu ya
mchezo, licha ya kuwa walikuwa nyuma.
URA walifanikiwa kupata goli la kusawazisha dakika
14 kabla ya mchezo kumalizika kupitia kwa Peter Lwassa,huku mabao yakiwa ni
Yanga 1-1 URA. Katika hatua ya mikwaju ya penati Geofrey Mwashiuya na Malimi
Busungu walikuwa hawana bahati, kwani walikosa penati, lakini URA mchezaji
aliyekosa penati alikuwa ni Sekito Sampekee. URA imeifuata Mtibwa Sugar fainali
kwa kuibuka na ushindi wa penati 4-3.
0 comments:
Post a Comment