Image
Image

Nahodha wa Gor Mahia Onyango sasa kujitosa kwenye siasa mwaka ujao, 2017.


Nahodha wa mabingwa wa soka nchini Gor Mahia Jerim Onyango atawania wadhifa wa kisiasa katika uchaguzi mkuu mwaka ujao, 2017.
Mlinda lango huyo, wa miaka mingi, alisema atawania kiti cha Mwakilishi wa Wadi (MCA) cha Ugunja katika eneo bunge la Ugunja, kaunti ya Siaya.
Jerim Onyango ambaye pia amewahi kuwajibia timu ya kitaifa, Harambee Stars, kama golikipa amesema sasa atalikunja jamvi lake kama mwanasoko baada ya kutafakari kwa kina na kuzungumza na wakazi wa Ugunja, na kuridhika kuwa huu ndio uamuzi mwafaka
Siku hizi ni nadra kwa Onyango kuchezeshwa kwani nafasi yake imekuwa ikipewa Boniface Oluoch aliyejiunga na Gor kutoka klabu ya Tusker.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment