Maalim Seif: Ingawa mwenyekiti aliitisha kikao kuhalalisha maamuzi yake bado tume haikuwa na mamlaka ya kuhalalisha maamuzi ya kufuta uchaguzi uliokamilika.
Tangazo rasmi lina kasoro zifuatazo, linasema tarehe 28 October tume ilikutana, tume haikukutana kabisa kwa vile mwenyekiti hakwenda kwenye kituo.
Migongano: Tamko la mwenyekiti lilisema anafuta uchaguzi na matokeo yake yote hata hivyo tangazo rasmi lilisema anafuta matokeo ya uchaguzi
Vingufungu vya katiba vilivyonukuliwa, vimenukuliwa kwa ubabaishaji kuhalalisha uwezo wa tume kufututa matokeo. Kifungu cha 34 kimeweka utaratibu wa kufunga kituo ikitokea dosari, sheria imetoa fursa ya wazi kwa mwenye malalamiko na kwa mujibu wa sheria hakuna malalamiko yaliyowasilishwa mbele ya tume.
Tangu uchaguzi wa vyama vingi zianze zimekuwa zimekumbwa na kasoro ukiwemo wa mwaka 2000 uliolazimu vituo 16 kurejea uchaguzi Zanzibar, hivi kweli uchaguzi wa 2015 ulizidi kasoro za mwaka 2000.
Tume kuingiliwa kazi zake: Tume haipaswi kupewa maagizo na chama chochote cha siasa au chombo chochote, ni dhahiri maamuzi ya mwenyekiti yalikuwa ya maagizo kama alivyowaeleza wenzake.
Athari za kufutwa kwa uchaguzi kumepelekea athari kadha za kikatiba, mgogoro mkubwa wa kikatiba na kisheria.
Imepelekea Zanzibar kuwa na mgogoro kwa Rais aliyeko madarakani, washauri wametumia tafsiri isiyo sahihi ya kikatiba hadi Rais mpya atakapoapishwa. Mpaka wa kifungu kinachorusu mpaka Rais ajae atakapoapishwa ni kuwa muda wa Rais ni miaka mitano pekee na katiba haijaruhusu muda wa miaka mitano uongezwe kiholela ila kwa masharti mazito ikiwemo vita na Rais akaona ni muhimu kusitisha uchaguzi basi ataitisha baraza la wawakilishi na linaweza kumuongezea muda usiozidi miezi sita.
Tafsiri isiyokuwa sahihi ina athari zifuatazo
- Haujawekwa muda maalum na katiba imeweka muda maalum kwa chaguzi zinazofutwa kisheria, kwa maana hiyo hakuna ukomo mpaka uchaguzi utapoitishwa tena.
- Tafsiri hio haimpi fursa ya Rais kumuwajibisha mtu alienda kinyume cha katiba kwa sababu imemnufaisha Rais. Tafsiri sahihi ni lazima Rais ashike madaraka ya Urais na aachie nafasi hio baada ya miaka mitano isipokuwa kwa dharura zilizopo kisheria.
Hadi sasa tumeshafanya vikao 8, nimekubali kuanya kikao ambacho mimi niko peke yangu na CCM wako nane lakini nilikubali ili kushirikisha marais wetu wastaafu. Hata hivyo inasikitisha kuona mimi nikikubali kuwa kimya kipindi chote, inasikitisha kuona viongozi wa upande mwingine wakiongea na kuwachanganya watu.
Magufuli pamoja na juhudi zote hakuacha kufitinishwa kwa Balozi Seif Ali Iddi kusema eti Magufuli kasema turudi Zanzibar kukamilisha taratibu za kurudia uchaguzi ilhali mimi hakuniambia.
Hadi jana ukiangalia tovuti ya uchaguzi Zanzibar hadi jana inasema uchaguzi ulifanyika kwa amani nchi nzima.
Ni wa zi Dr Ali Shein hakua na nia njema na mazungumzo haya na amepoteza sifa ya kuongoza mazungumzo haya. Tunazo taarifa tume ya uchaguzi imepanga kukutana January ili kutangaza kurudiwa kwa uchaguzi. Wananchi wa Zanzibar wako taaban na wamekumbwa na fadhaa baada ya kuona maamuzi yao yanakanyagwa.
Hitimisho
Zanzibar imepita siasa za dhoruba na machafuko kwa miaka 50 ndio maana mimi mwaka 2009 na Rais mstaafu Karume tulifikia maridhiano. Tuanzungumza na watanzania na kuwajuvya haya. Ni bahati mbaya sana wengine wanachukulia uungwana wetu kama ni udhaifu.
Zanzibar kuna tatizo kubwa ambalo halipaswi kuendelea kupuuzwa, Nawashukuru sana.
==============
Maswali:
Bakari: Unahisi kwanini CCM wanasema lazima kwamba lazima uchaguzi urudiwe
Kuna taarifa kwamaba mmeshakubaliaana lazima uchaguzi urudiwe na unaona utaitwa msaliti.
Meena: Una uhakika gani huyu Magufuli unayemsema unamuamini kama ulivyomtanguliza
Majibu:
Mimi kama Seif siwezi kufanya maamuzi, lazima tuitishe kikao cha kufanya maamuzi. CUF sio Seif, ina wenyewe.
Kwanini CCM ina ujasiri? Dhana yangu wanaringia vyombo vya dola, wanadhani wanaweza kufanya lolote na vyombo vya dola vitawakingia kifua. Umma ukiamua hakuna chombo cha dola kitachopinga, hatutaki tena yatokee yaliyotokea 2001.
Mimi ni mtu najiamini, nikichukua maamuzi nayatangaza. Sina haja ya kuficha, mimi naongozwa na maslaha ya nchi yetu basi na mwisho utaona msimamo wangu. Naamini uchaguzi unaweza ukaleta vurugu Zanzibar, watatufikisha mahala ambako sisi hatutaki tufika.
Kama mimi si mzinzibari, chaguzi tano nagombea urais na hakuna mtu hata mmoja anaweka pingamizi, hata kumjibu ni kinyaa. Eti Zanzibar vyama vya upinzani viruhusiwe kugombea nafasi zote kasoro Urais, wanaogopa nini? Wote ni watanzania na wanaogombea kupitia vyama hivyo ni watanzania.
0 comments:
Post a Comment